Bodaboda msilie wala kuumia, CHADEMA haioni umuhimu wenu lakini CCM inawajali na kuwaheshimisha

Nitajie mkubwa wa CCM ambaye mtoto wake Ni bodaboda.
Watoto wao Ni special for teuzi na kufanya biashara bila kulipa Kodi halafu wanakuambieni mchemke na pikipiki Ni kazi ya heshima.
Kalaga baho.
 
Bodabodaa wako duniani kote, inamaana Nako uko wamelaaniwaa?? Vijana wameacha shuli zao za kuingiza kipato Kwa ajiri ya kulelea watoto wao, na kuja kumpokea ndugu Yao, halafu wanaambulia kutukana eti WAMELAANIWA?
Hata wakulima wako duniani kote lakini wakulima wa vijiji vya Tanzania hawalinganishwi na china, cuba, marekani nk. Hii ni bongo imekaa kibongobongo
 
Huwezi kulisaidia kundi la vijana kwa ajira rasmi pekee utakuwa unawadanganya. Vijana ni kundi kubwa ambapo inajumuisha wasomi sana, wasomi wa Kati na wasio wasomi hivyo huwezi kushughulikia kundi kubwa hivi kwa ajira rasmi ni lazima mikakati ya kuwashauri wajiajiri iwepo.

Moja ya njia ya vijana kujiajiri ni kupitia bodaboda na wengine Wana maisha mazuri sana kupitia kazi hii. Kupitia kazi hii tunaona amani ikiwepo mtaani sana na vijana Wana furaha sana. CHADEMA msiwadanganye vijana kwamba mkipewa dola mtaweza Kuwapatia vijana wote ajira
Wewe ni chizi aisee
 
Marekanii wapo Hadi kanada alipokuwa kema, bodabodaa Bado wapooo. Hata kama wawepo kwenye inchi masikini, ndio uwatukane kwamba wamelaaniwaa?? Huyu KIJANA awatake radhi bodabodaa wetuuu. Watu wamempokea Kwa shangwe na nderemo halafu wanaambiwa eti wamelaaniwaa? Kweliii??
Ni sawa na kusema jf kuna great thinkers lakini kumbe kuna mtu kama wewe pia
 
Sio rahisi kukielewa alichosema Lema kama hutotumia mlango wa sita wa fahamu au jicho la tatu kukitafakari kwa makini lakini yote kwa yote bodaboda wamefedheshwa sana.

Mwenye kulaani na kubariki ni Mungu pekee na mafundisho ya kiimani yanafundisha juu ya kuongezewa kwa kile ulichonacho. Bodaboda ni kazi ambayo Mungu anambariki mwenye nayo na mwanadamu kumlaani mwenye kuifanya ni kuonesha mipango ovu mtu aliyonayo kwa sababu binafsi.

MTAZAMO WANGU
Binafsi ninaamini maneno ya Lema juu ya bodaboda ni mkakati wa CHADEMA na sio maneno tu kwa sababu bodaboda ni kundi linaloiamini sana CCM na kwa jicho la tatu unaona Kuna mpango wa kulifarakanisha kundi hili na CCM ili CCM ikose ushawishi nawaombia mtashindwa na hamtoweza. Jicho la tatu linaona sio bodaboda tu wanaolengwa na CHADEMA baada ya hapa watakuja kwa machinga, mama ntilie n.k

Kwangu, hii ni agenda ya upinzani kuwafitinisha Wananchi. Wanalenga makundi makubwa na yenye ushawishi kwa CCM. Hakuna mtu timamu mwenye kuweza kuilaani kazi na shughuli halali ya mtu from nowhere bila Jambo kuwa na faida kwake.

USHAURI KWA BODABODA
Poleni sana kwa dhihaka kubwa mliyopewa na CHADEMA ninatambua hawaoni umuhimu wote na Mara nyingine mnatumiwa kwenye shughuli zao bila kulipwa na hii ni kuwadharau sana.

Msilie wala msilalamike CCM ni chama kinachowajali na kuwaheshimisha. Toka serikali ya awamu ya nne mpaka CCM ipo pamoja na bodaboda.

Tumieni umoja wenu kuwaonesha wale wanaowadharau na kushindwa kuona umuhimu wenu ninyi ni jeshi kubwa. Pia, ninawashauri muendelee kujirasimisha na kuunda umoja wenye kwa ajili yenu.

USHAURI KWA CCM
Kwa kuwa kile CHADEMA kimeona vijana hawa hawafai , hii kwenu ni fursa ya kuwajengea imani juu ya CCM. Wahakikishieni shughuli zao ni baraka na sio laana. Wawezesheni kwa mafunzo ya usalama barabarani na utumiaji salama vyombo vyao ,wahimizeni kujirasimisha na mwisho shirikianeni nao kwenye mipango ya maendeleo.

Kazi ni kipimo Cha utu ni Imani ya CCM.

Ni Mtetezi wa bodaboda na machinga
Heee!umelipwa nyingi

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Fursa za kuwapa Ajira vijana ziko nyingi, tena Kwa kuanzia vijana wasomi

Kuna vijana wasomi wa IT na Wana office zao na wanafanya kazi ndogo ndogo Sana, why serikali isiwe inatumia kampun za hao vijana kufanya mambo ya computer kwenye taasisi zake? Unaona Hilo haliwezekani?

Kuna vijana wasomi Wana kampun ndogo ndogo za printing kwenye tishet, na graphics

Why nyie ccm msiwatumie hawa vijana kufanya printing za mabango yenu na tishet zenu na badala yake mnawapa wachina?

Janga la vijana linakuwa kubwa because ya uzembe ambao uko somewhere tu

Wanataka vijana wawe boda au waende manispaa wakiwa group la watu 50 wakapewe milion 2 wafuge Kuku au samaki

Me naungana na lema, kazi ya bodaboda ni kazi ya laaana
Zungumzia vijana wasio wasomi wanasaidiwa vipi kwenye ajira rasmi ?kwa vijana wasomi kila siku serikali inatengeneza mazingira ya kuwaajiri lakini vipi wale wasio wasomi ambalo ni kundi kubwa zaidi.
 
Serikali inachofanya Kwa vijana wasomi ni kuwaambia wajiunge vikundi vya watu 20 waende Kwa mkurugenzi wa halmashauri yao wakachukue 2M wafuge samaki, kuku, sungura, hakuna la zaidi hapo

Vijana ambao sio wasomi msaada wao ni kuwapa project Tu, hawa wachina wengi ambao unawaona Africa ni vijana ambao hawana Ajira huko kwao so serikali inaweka kwenye makampuni ya china au ya nje ya china

Jaribu kuwaza Nani amepata tenda ya kufagia barabara? Nani amepata tenda ya kusafisha office za serikali?

Kwanini hizo mambo wasipewe vijana ambao hawana shule?

Why wasijiunge vikundi vya watu 20 wakapewa vifaa vya usafi na barabara then wakalipwa kama wanavyolipwa hao ambao wamechukua tenda?
 
Zungumzia vijana wasio wasomi wanasaidiwa vipi kwenye ajira rasmi ?kwa vijana wasomi kila siku serikali inatengeneza mazingira ya kuwaajiri lakini vipi wale wasio wasomi ambalo ni kundi kubwa zaidi.
Hayo mazingira yametengenezewa wapi?
Kwani wewe unaishi wapi huko ambako kilasiku serikali inawaajiri vijana? Upo Tanzania kweli?
 
Bodabodaa wako duniani kote, inamaana Nako uko wamelaaniwaa?? Vijana wameacha shuli zao za kuingiza kipato Kwa ajiri ya kulelea watoto wao, na kuja kumpokea ndugu Yao, halafu wanaambulia kutukana eti WAMELAANIWA?
Naweza kusema ni kweli,Sababu bodaboda wengi Inchi wanazohangaika,Viongozi wake ni wezi wa kutupa kama Tanzania,badala ya kuwatengenezea uchumi na ajira wananchi wao, wenyewe wanaishia kujilipa mishahara mikubwa kutembelea magari ya anasa maV8,na kuiba hera kuficha inje ya inchi,halafu wanajifanya kuwapanga mafuta kwa mgongo wa chupa bodaboda wetu
 
Sio rahisi kukielewa alichosema Lema kama hutotumia mlango wa sita wa fahamu au jicho la tatu kukitafakari kwa makini lakini yote kwa yote bodaboda wamefedheshwa sana.

Mwenye kulaani na kubariki ni Mungu pekee na mafundisho ya kiimani yanafundisha juu ya kuongezewa kwa kile ulichonacho. Bodaboda ni kazi ambayo Mungu anambariki mwenye nayo na mwanadamu kumlaani mwenye kuifanya ni kuonesha mipango ovu mtu aliyonayo kwa sababu binafsi.

MTAZAMO WANGU
Binafsi ninaamini maneno ya Lema juu ya bodaboda ni mkakati wa CHADEMA na sio maneno tu kwa sababu bodaboda ni kundi linaloiamini sana CCM na kwa jicho la tatu unaona Kuna mpango wa kulifarakanisha kundi hili na CCM ili CCM ikose ushawishi nawaombia mtashindwa na hamtoweza. Jicho la tatu linaona sio bodaboda tu wanaolengwa na CHADEMA baada ya hapa watakuja kwa machinga, mama ntilie n.k

Kwangu, hii ni agenda ya upinzani kuwafitinisha Wananchi. Wanalenga makundi makubwa na yenye ushawishi kwa CCM. Hakuna mtu timamu mwenye kuweza kuilaani kazi na shughuli halali ya mtu from nowhere bila Jambo kuwa na faida kwake.

USHAURI KWA BODABODA
Poleni sana kwa dhihaka kubwa mliyopewa na CHADEMA ninatambua hawaoni umuhimu wote na Mara nyingine mnatumiwa kwenye shughuli zao bila kulipwa na hii ni kuwadharau sana.

Msilie wala msilalamike CCM ni chama kinachowajali na kuwaheshimisha. Toka serikali ya awamu ya nne mpaka CCM ipo pamoja na bodaboda.

Tumieni umoja wenu kuwaonesha wale wanaowadharau na kushindwa kuona umuhimu wenu ninyi ni jeshi kubwa. Pia, ninawashauri muendelee kujirasimisha na kuunda umoja wenye kwa ajili yenu.

USHAURI KWA CCM
Kwa kuwa kile CHADEMA kimeona vijana hawa hawafai , hii kwenu ni fursa ya kuwajengea imani juu ya CCM. Wahakikishieni shughuli zao ni baraka na sio laana. Wawezesheni kwa mafunzo ya usalama barabarani na utumiaji salama vyombo vyao ,wahimizeni kujirasimisha na mwisho shirikianeni nao kwenye mipango ya maendeleo.

Kazi ni kipimo Cha utu ni Imani ya CCM.

Ni Mtetezi wa bodaboda na machinga
ccm inawajali na kuwaheshimisha bodaboda kwa lipi
 
CCM inastawi Kwenye Umaskini na Ujinga.
Hivi Vitu ukivipunguza CCM inakufa.
 
Acha kuwapumbaza, hao viongozi wa CCM mbona wanawapa vyeo watoto na wajukuu zao, madukani bodaboda zipo nyingi tu kwanini hawawanunulii wafanye kazi hizo kama ni nzuri.
Kwa kweli bodaboda siyo kazi ya kuitegemea maisha yako yote na wala hakuna mzee aliyefundisha mwanawe na kutarajia kuwa siku moja atakuwa bodaboda.
 
Nimejaribu kukutana na bodaboda wasomi kiukweli wamempuza lema si mchezo
 
Naweza kusema ni kweli,Sababu bodaboda wengi Inchi wanazohangaika,Viongozi wake ni wezi wa kutupa kama Tanzania,badala ya kuwatengenezea uchumi na ajira wananchi wao, wenyewe wanaishia kujilipa mishahara mikubwa kutembelea magari ya anasa maV8,na kuiba hera kuficha inje ya inchi,halafu wanajifanya kuwapanga mafuta kwa mgongo wa chupa bodaboda wetu
Kwahiyo ndio sababu KIJANA wenu ya kuwatukana waendesha bodaboda WAMELAANIWA??
 
Hivi ni mtoto wa kiongozi gani anayeendesha boda?
Sijawai kuona mtoto wa kiongozi yeyote akiendesha bodaboda.
Lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Lema kajikwaa kwenye maneno
 
Back
Top Bottom