Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Kupunguzwa kwa kodi za vyombo vya usafirishaji kumewaletea nafuu maafisa usafirishaji mkoani hapa, hali iliyowasukuma kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwatengenezea mazingira rafiki ya kazi.
Akiwasilisha shukrani kwa niaba ya maafisa usafirishaji wenzake, Mweka Hazina wa Chama cha Usafirishaji Wilaya, Joseph Zebedayo, ametoa pongezi hizo wakati wa hafla ya kukabidhi bajaji 10 za umeme kwa vijana.
Zoezi hilo limeendeshwa chini ya usimamizi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, ambaye amewahakikishia maafisa usafirishaji, katika kipindi cha uchaguzi, watapatiwa vizibao maalum vitakavyowatambulisha wanapokuwa barabarani nyakati za usiku.