Bodaboda na Walimu wote ni madaraja ya wanasiasa kufikia malengo yao

Kwitogelo

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2023
Posts
310
Reaction score
442
Kipindi cha kampeni bodaboda hufanya amsha amsha ya mitaa na kuhadaiwa na wanasiasa kuwachagua kwa ahadi fulani.

Baada tu ya uchaguzi kuisha hudharauriwa na wanasiasa kama walivyodharauriwa na Lema.

Walimu hawa kazi yao haitofautini sana na bodaboda katika kuwafikisha wanasiasa pale wanapotaka kufika kisiasa.

Ndugu zetu hawa hutumia elimu zao na ushawishi wao kuanzia kwa wanafunzi mpaka kwa jamii (nje ya mazingira ya shule) na wanafunzi na jamii kwa ujumla huamini kile wanachoambiwa na walimu.

Baada tu ya uchaguzi kupita kudharauriwa ndo kama hivi hadi bodaboda nae anamdharau kiasi hiki na kusahau kwamba aliyeanzisha dharau dhidi yao(bodaboda) syo mwalimu bali ni mwanasiasa.

Bodaboda acheni dharau dhidi ya mwalimu, wote kwa wanasiasa nyie ni madaraja kwao!!!
 
Tayari wanasiasa wa ccm wamepata pointi ya kujipendekeza kwa bodaboda na vicoba wakimtwanga lema kwa kauli yake juu ya bodaboda na vicoba. Wanasiasa wanapenda sana cheap popularity
 
Walimu wana njaa kali sana, wale imezoeleka ndio taraja la wanasiasa, mbaya zaidi walimu wenzao wanaochomoka na kuingia siasani huwasaliti wenzao na kuwatumia kisiasa wafikia malengo yao
 
Daa ukweli siku zote huwa kama muhogo mchungu!!
Walimu ni watu wakujiona wameyapatia maisha,nimeishi pia nafanya kazi nao!!
 
Kipindi cha kampeni bodaboda hufanya amsha amsha ya mitaa na kuhadaiwa na wanasiasa kuwachagua kwa ahadi fulani.

Baada tu ya uchaguzi kuisha hudharauriwa na wanasiasa kama walivyodharauriwa na Lema.

Walimu hawa kazi yao haitofautini sana na bodaboda katika kuwafikisha wanasiasa pale wanapotaka kufika kisiasa.

Ndugu zetu hawa hutumia elimu zao na ushawishi wao kuanzia kwa wanafunzi mpaka kwa jamii (nje ya mazingira ya shule) na wanafunzi na jamii kwa ujumla huamini kile wanachoambiwa na walimu.

Baada tu ya uchaguzi kupita kudharauriwa ndo kama hivi hadi bodaboda nae anamdharau kiasi hiki na kusahau kwamba aliyeanzisha dharau dhidi yao(bodaboda) syo mwalimu bali ni mwanasiasa.

Bodaboda acheni dharau dhidi ya mwalimu, wote kwa wanasiasa nyie ni madaraja kwao!!!
Uliwahi muona bodaboda amejengewa nyumba na Serikali?
 
Back
Top Bottom