BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Bodaboda wamekuwa kero kubwa na kusababisha ajali za mara kwa mara kwenye njia hiyo kutokana na kuwa na uharaka ambao hauzingatii Usalama wa Raia.
Kibaya zaidi alama maarufu kama 'Zebra' kwenye kipande hicho zimefutika jambo ambalo limeongeza kero zaidi na kufanya Bodaboda wengi washindwe kusimama au kupunguza mwendo kasi, huku abiria wakiwa wanakatiza eneo lolote.
Ni vyema mamlaka za Jiji zikaiona kero hiyo na kushirikiana na Askari wa Barabarani 'Traffic' kuweka utaratibu rafiki ambao utaondoa kero hiyo hususani kuweka vibao vya msisitizo kwa bodaboda kuzingatia usalama wa raia pamoja na usalama wao binafsi inapotokea wametumia njia hiyo kwa dharura.
Pia alama za zebra kwenye eneo hilo ni vyema zikakolezwa zaidi ili ziweze kuonekana kwa uharaka jambo ambalo litasaidia wananchi kutokatiza ovyo ovyo kwenye kipande hicho chenye harakati nyingi pande zote mbili.
Bila kuwajibika kuchukua hatua tutaendelea kuwa tunaweka hatarini maisha ya raia wengi na inweza kuja kutokea janga kubwa zaidi ambalo kimsimgi kutowajibika kwetu kwa wakati inaweza kuwa kisababishi.