mlinzi mlalafofofo
JF-Expert Member
- Apr 20, 2008
- 725
- 1,282
Sasa hivi jamaa wanaleta vitimbi vyao hadharani na hamna kitu unaweza kuwafanya.
Ni kama wana utawala wao wapo Dunia yao isiyo na Sheria. Wao ndio mabingwa wa kubebana mishikaki na kuchomekea wengine kwa mbele kwa kisingizio cha wana haraka.
===========
Bodaboda sehemu nyingi hawakai kwenye foleni, hata kwenye Taa za Barabarani wao wanachoangalia ni kwamba kuna kikao? Kama hakuna wanaamsha na kupita bila kujali ni zamu ya upande wao au la!
Wanapita sehemu ambazo sio wanazotakiwa kupita, mfano kwenye njia ya Mwendokasi au kwenye service Road tena wakiwa speed.
Ukienda kwenye vituo vya Afya kama vile MOI, unakuta watu wengi wakiwa na majeraha makubwa na wengine wamepoteza maisha wengine wamekuwa na ulemavu wa kudumu kutokana tu na tabia zao ambazo ni chanzo cha ajali nyingi.