PreGE2025 Bodaboda waaswa kutotumika kisiasa mwaka huu wa uchaguzi

PreGE2025 Bodaboda waaswa kutotumika kisiasa mwaka huu wa uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Maafisa Usafirishaji (Madereva bodaboda) wametakiwa kupambana dhidi ya vitendo vya rushwa kwa kutokuwa tayari kutumika kwa namna yoyote katika vitendo vya rushwa katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi mkuu 2025.

Wito huo umetolewa leo Aprili 17, 2025 na Mkuu wa Dawati la Elimu kwa Umma TAKUKURU mkoa wa Kigoma Bw. Ibrahim Sadick katika semina ya TAKUKURU na Viongozi wa vijiwe vya Bodaboda manispaa ya Kigoma Ujiji.

Pia soma Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akizungumza katika semina hiyo Ibrahim amesema wanasiasa wengi katika kipindi hiki cha uchaguzi wanalenga kulitumia kundi la Bodaboda kwani wanaamini ni kundi lenye changamoto nyingi na linaweza kutumika kiurahisi.

"Wanasiasa wengi sasahivi wanatambua na macho yao wameelekeza kwetu kwamba hili ndo kundi ambalo tukilipelekea ajenda ndogo kwa sababu lina changamoto nyingi basi tukatumie changamoto zao kama mtaji wetu wa kisiasa" Amesema Bw. Ibrahim.

Nao baadhi ya Viongozi wa vijiwe vya Bodaboda walioshiriki semina hiyo wameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kubuni mbinu mpya za mapambano dhidi ya rushwa na kuendelea kuishirikisha jamii katika mapambano hayo.

Kuhusu usalama wa mtoa taarifa Viongozi hao wameiomba TAKUKURU kuendelea kuimarisha usalama wa mtoa taarifa za vitendo vya rushwa kwani walio wengi hushindwa kutoa taarifa kwa kuhofia usalama wao.

Semina hiyo imefanyika ukiwa ni mwendelezo wa Programu ya TAKUKURU rafiki inayotekelezwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Kigoma.
 
Back
Top Bottom