Bodaboda wavamia ofisi ya Serikali ya Mtaa Tabata, wamchukua mwizi wa Bodaboda watokomea naye kusikojulikana

Ila bodaboda wakikudaka kwenye 18 zao umeisha. Hawa jamaa hawanaga simile wanakuua ASAP.

Kuna yule jamaa tanga alikua anaburuzwa kwenye kokoto, kuchoma moto kwao ni kawaida kabisa.

Ila wezi wa bodaboda ni washenzi sana, wanamuua boda halafu wanaenda kuiuza laki 5, uhai wa mtu laki 5 kweli.
 
Pengine hao ni wezi wenzake wamekuja kumtorosha kijanja.
 
Buda boda huwa wanahisi dunia hii imeumbwa kwa ajili yao?
Wanapora watu cmu mchana kweupe watu wanawaangalia tu
 
Rushwa aliozoea kuhonga imemponza
 
Inaonekana Sasa hivi watu hawana Imani kabisa na Vyombo vya utowaji wa haki Tanzania ndiyo maana wananchi wenye hasira kali wanajichukulia Sheria mkononi! Na pia ukisoma maoni ya wachangiaji wengi hum nao wanauunga mkono watu kujichukulia Sheria mkononi! Vyombo vyetu vya utowaji wa haki kuanzia police, waendesha Mashitaka pamoja na Mahakama inabidi wajipime kwa hayo matukio ya kujichukulia Sheria mkononi kabla hali haijakua mbaya zaidi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…