Bodaboda wavamia ofisi ya Serikali ya Mtaa Tabata, wamchukua mwizi wa Bodaboda watokomea naye kusikojulikana

Hii ya Viongozi kusema eti Wananchi wasijichukulie sheria mkononi hua ni kama formality tu na msemo wa kisiasa.

Wao wenyewe huibiwaga na mdomoni anasema tusichukue sheria wakati moyoni anasema "piga na ua kabisa umbwa huyo". Hata wao hawataki kusumbuka ma kesi kila siku.
 
wamekosea kumuua wezi wa pikipiki ni chain ndefu, kuna mwizi na kuna anayezinunua na kuzichinja spea na duka zinakopelekwa.
Sasa yule mnunuaji atatafuta mchongo kwa wezi wingine wizi utaendelea
Kweli, hii angeungiwa chain wadosi wawili watatu mtaani, na kuvamiwa na nyomi ya bodaboda, hii biashara ingekoma au walau kupungua.
 
Mwizi ni haki yake kuuawa
Mwizi yupi,wa bodaboda ya mil.2 au hata wale wanaoiba mabilioni?maana hawa wanaoiba mabilioni sijawahi kusikia wananchi wamechukua sheria mikononi ila ni kwa hawa wezi wa kuku na viatu...
 
Mwizi yupi,wa bodaboda ya mil.2 au hata wale wanaoiba mabilioni?maana hawa wanaoiba mabilioni sijawahi kusikia wananchi wamechukua sheria mikononi ila ni kwa hawa wezi wa kuku na viatu...
Tofauti iliyopo huyu mwizi wa bodaboda haiishii tu kuiba bodaboda ukicheza hata wewe atakutoa uhai, Hana chembe ya huruma kabisa hata kama hiyo bodaboda ataiuza 200k lakini Yuko tayari akutoe uhai aichukue
 
Watu wengi hawajui hilo.
Unataka Pikipiki ya 2m,mtu anakupiga na shoka au hata chuma kizito.
Wameua Vijana wengi sana ambao pia wana Familia.
2M ni ya kuua mtu kwa Shoka tena mapema tu jioni.
Boda boda wengi siku ni vijana wana Diplom na Degree,kuna baadhi ya vijiwe wapo Elite sana.Wanataratibu ngumu hat huku Maofisini hakuna.

Hii ni kulinda maisha yao.

Hata huko kwenye Bajaj,na ndio maana wana Intel zote za wizi na kila aina ya ushenzi.
Hizi zimekuwa kazi kama kazi zingine.Ikumbukwe kama Boda na Bajaji zisingekuwepo vijana wengi wangekuwa wezi na mtaani huku kungekuwa kugumu sana.

Japo baadhi yao pia wamekuwa wezi tokana hulka zao na tabia.
 
Polisi wamejirudi, wizi utapungua.
 
Mwizi sio wa kumchekea, haswa Hawa wa bodaboda, ni kuua Mara 1 kenge Hawa, wanaua vijana(bodaboda) kikatili mnoo
 
Kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…