SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Wakuu,
Biashara ya bodaboda imekuwa mkombozi kwa kurahisisha usafiri katika maeneo mengi nchi hii, mijini na hata nje ya miji.
Lakini pia imekuja na mambo mengi maovu, kama vile kutumika katika ujambazi na unyang'anyi ukiachilia mbali ajali nyingi zinazosababisha ulemavu wa kudumu hata vifo kwa madereva na abiria.
Hata hivyo, mada yangu inaangalia zaidi mmomonyoko wa maadili unaotokana na jinsi dereva na abiria wanavyokaribiana viungo vyao wakati wa safari. Hapa sitazingatia jinsia za abiria au dereva maana nadhani athari zake ni zile zile.
Mfano mimi ni mwanaume 😎😎, leo asubuhi nimepanda bodaboda, alipofika nikagundua amevaa boxer tu bila suruali au nguo nyingine juu yake. Kwa kuwa siko huko na sijaumbwa kumuwazia mwanaume mwenzangu, nikawaza tu, je uvaaji wa namna ile una maana gani? Je, hauwezi kuwaathiri wengine, abiria au hata dereva mwenyewe?
Na ni vipi wanaume watatu au wakati mwingine wanne wanapobanana katika style ya mishkaki! Hili nalo halina athari kweli za muda mrefu kwa watu hawa kimaadili?