Bodaboda zinachangia kumomonyoka kwa maadili

SAYVILLE naona labda kama kuna kitu ulitaka simulia tu. Haiwezekani bodaboda awe na boxer tu nawe ukakubali akuendeshe na njia nzima trafik au polisi wamtizame tu.Ungesema wamekuwa makuwadi kuuza wanawake au wapeleka sehemu za maaasi na ujambazi hapo ningekuelewa lakini hili mla boxer tupu mhh bado haiingii akilini
 
Mkuu sitanii kwenye hili. Nilivyokuwa napanda niliona kama ni boxer kwa sababu ya ufupi na rangi yake, nikasema embu ngoja nitaangalia vizuri nikishuka. Nilivyokuwa nashuka nikaangalia vizuri nikajihakikishia kabisa. Na ilikuwa mida ya asubuhi sana kwa hiyo uwezekano wa kuwa ndiyo ameamka tu akasema akatafute hela ya chai ndiyo arudi kuvaa ni mkubwa!

Kuna watu wanaishi maisha ya ajabu sana hapa mjini, we acha tu.
 
Bodaboda alikaaje hapo kijiweni na boxer tupu bila suruali!
 
Kuna kitu ulitaka kueleza ila umeishia jujuu sana. Mfano. Hujasema kuhusu ulevi, speed, kupiga honi bila sababu nk
 
Inasikitisha sana...

Hapo wewe ukichowaza nini, baada ya kuona jamaa ana boxer?
Acha mambo ya ajabu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…