Bodi ya Ligi imetumia kanuni gani kuahirisha mchezo wa derby?

Simba wameogopa kucheza na yanga kwa kipindi hiki. Sababu zingine ni blah blah tu.
 
 
Kwanza,tuelewe kuwa timu hizi mbili simba na yanga ni timu kubwa si tu Tanzania bali kimataifa hasa hapa Afrika na dunia kwa ujumla hivyo ni timu hizi zinafanya soka letu linakuwa zaidi ningewaomba wachezaji,kamati za kiufundi mfn mabenchi yote ya timu hizi mbili na uongozi wa TPL kutengeneza umoja na mungaano ili kuachana na adha za migogoro ya vilabu vyetu pendwa hapa nyumbani Tanzania. Pia machizi soka wa mpira tuelewe kuwa mpira ni burudani na siyo sehemu ya kuzalisha vita,wasama na hila zinazo weza kuleta matokeo hasi kwa jamii,vilabu vyetu na kwa uchumi wa Taifa letu.
 
Kwa hili limeshatokea hatuna budi kukabiliana nalo lakini limeweka dosari kwenye ligi yetu hapa Tanzania bara,TPLB wafanye kutangaza tarehe ya mchezo huo na kuwaonya wote watakao patikana na hatia kwa mjibu wa kanuni,taratibu na sheria zinazoingoza TPLB katika kutoa haki na kuendesha ligi yetu ya NBC Premium league
 
Kanuni au Sheria yoyote itakayovunjwa adhabu ya chini iwe milioni 500, kama kanuni itahusu judhibiti vitendo vya kishirikina adhabu si chini ya 1 billion na kupokea point 5. Lengo kukomesha tabia na Imani za kilozi.
 
Kimsingi ni uhuni uliofanywa kwa ushirikiano wa Simba, TFF na TPLB ,kuahirishwa mchezo hip.

Simba ,TFF na TPLB ni Taasisi ambazo zipo kisheria, na mechi ya Ligi kuu ipo kisheria.

Haiwezekani wahuni ambao wanaitwa mabaunsa wazuie Taasisi 3 kufanya Kazi zao ambazo zipo kwa mujibu wa sheria! Haiwezekani!


Mabaunsa ni nani hadi wawe na nguvu kushinda Taasisi zilizo wekwa kwa mujibu wa sheria !
Haiwezekani nguvu ya Simba, TFF na TPLB washindwe kudhibiti wahuni wanao itwa mabaunsa, pale pale kwa Mkapa kuna Police Post, Chang'ombe Police ni jirani, inawezekana vipi wahuni wazuie Kazi halali kufanyika wakati vyombo vya usalama vipo .

Kuna kitu kinafichwa , Simba walijua hawako tayari kuwa derby ,walitafuta sababu tu za kutocheza mpira, kwa kushirikiana na TFF na TPLB, huyo ndio dhana yangu
 
Wametumia busara kutoka juu huko kwenye system, ambazo zimesababisha bodi kwasasa Iwe na kigugumizi wanasubiri hiyo hiyo system itoe maelekezo baada ya kuchafua hali ya hewa, kikikiki

Kwakifupi bodi ya ligi hamna kitu wamedhihirisha kwamba wapo kama sanamu, (figure heads)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…