Bodi ya Ligi imetumia kanuni gani kuahirisha mchezo wa derby?

Bodi ya Ligi imetumia kanuni gani kuahirisha mchezo wa derby?

Sijaona kuna kanuni gani hapo inayosema mchezo unatakiwa kuahirishwa. Mbona mchezo wa JKT Queens haukuahirishwa? Vipi mchezo wa Boashara utd? Pamba?

NB; kama haujui, mchezo hautakiwi kusimamishwa, lazima mchezo uchezwe ila hatua na adhabu hufuata baada ya mchezo.
Simba wameogopa kucheza na yanga kwa kipindi hiki. Sababu zingine ni blah blah tu.
 
Adhabu ya kufanya usumbufu wowote kupelekea timu pinzani kushindwa kufanya mazoezi ni Tsh 1 milion mpaka 5 million, Lakini hayo yote hufanyika na kamati ya saa 72 BAADA ya mchezo husika (sio kabla ) Kwa maana nyingine LAZIMA mchezo uchezwe kwanza, Haya hiyo kanuni ya kusena mchezo hauchezwi Bodi ya Ligi imetoa wapi?
1000256222.jpg
 
Kwanza,tuelewe kuwa timu hizi mbili simba na yanga ni timu kubwa si tu Tanzania bali kimataifa hasa hapa Afrika na dunia kwa ujumla hivyo ni timu hizi zinafanya soka letu linakuwa zaidi ningewaomba wachezaji,kamati za kiufundi mfn mabenchi yote ya timu hizi mbili na uongozi wa TPL kutengeneza umoja na mungaano ili kuachana na adha za migogoro ya vilabu vyetu pendwa hapa nyumbani Tanzania. Pia machizi soka wa mpira tuelewe kuwa mpira ni burudani na siyo sehemu ya kuzalisha vita,wasama na hila zinazo weza kuleta matokeo hasi kwa jamii,vilabu vyetu na kwa uchumi wa Taifa letu.
 
Kwa hili limeshatokea hatuna budi kukabiliana nalo lakini limeweka dosari kwenye ligi yetu hapa Tanzania bara,TPLB wafanye kutangaza tarehe ya mchezo huo na kuwaonya wote watakao patikana na hatia kwa mjibu wa kanuni,taratibu na sheria zinazoingoza TPLB katika kutoa haki na kuendesha ligi yetu ya NBC Premium league
 
Kanuni au Sheria yoyote itakayovunjwa adhabu ya chini iwe milioni 500, kama kanuni itahusu judhibiti vitendo vya kishirikina adhabu si chini ya 1 billion na kupokea point 5. Lengo kukomesha tabia na Imani za kilozi.
 
Kilichotokea leo ni ujinga na uhuni na ni uthibitisho wa ombwe kubwa la uongozi tulilonalo.Soka la nchi hii tumewaachia wahuni waliendeshe na haya ndio matunda yake.Ni bora kubaki kushabikia timu za ulaya zinazosimamiws na Watu wanaojitambua na kuheshimiana sio huu upuuzi wa Simba na Yanga.Hakika mnakera na mnakosa heshima kwa Mashabiki.Si Simba si Yanga wote mnaleta sababu za kitoto kana kwamba nasi Mashabiki ni Watoto wenzenu.Mimi ni Simba lakini nitaridhia tukipoteza pointi tatu zote kama adhabu.Mnawaponza na Wachezaji wasio hatia,wamejiandaa alafu kirahisi tu mechi hakuna.Tungekuwa na Viongozi makini kusingekuwa na huu ujinga ujinga.
Kimsingi ni uhuni uliofanywa kwa ushirikiano wa Simba, TFF na TPLB ,kuahirishwa mchezo hip.

Simba ,TFF na TPLB ni Taasisi ambazo zipo kisheria, na mechi ya Ligi kuu ipo kisheria.

Haiwezekani wahuni ambao wanaitwa mabaunsa wazuie Taasisi 3 kufanya Kazi zao ambazo zipo kwa mujibu wa sheria! Haiwezekani!


Mabaunsa ni nani hadi wawe na nguvu kushinda Taasisi zilizo wekwa kwa mujibu wa sheria !
Haiwezekani nguvu ya Simba, TFF na TPLB washindwe kudhibiti wahuni wanao itwa mabaunsa, pale pale kwa Mkapa kuna Police Post, Chang'ombe Police ni jirani, inawezekana vipi wahuni wazuie Kazi halali kufanyika wakati vyombo vya usalama vipo .

Kuna kitu kinafichwa , Simba walijua hawako tayari kuwa derby ,walitafuta sababu tu za kutocheza mpira, kwa kushirikiana na TFF na TPLB, huyo ndio dhana yangu
 
Kwa mujibu wa kanuni zinazoendesha bodi ya Ligi, hizi ndizo sababu pekee zinazoweza kusababisha mchezo wa Ligi kuu kuahirishwa.

KANUNI YA 9
KUAHIRISHA MCHEZO
Mchezo unaweza kuahirishwa kutokana na sababu yoyote kati ya zifuatazo:-
(a) Endapo timu ina wachezaji watano au zaidi katika timu ya Taifa;
(b) Endapo timu inashiriki katika mashindano ya Kimataifa na ina muda usiozidi siku sita kufikia mchezo wa Kimataifa;
(c) Sababu yoyote ya dharura nzito na yenye msingi itakayokubaliwa na TFF
(d) Mchezo wowote ulioahirishwa utapangwa tena katika tarehe itakayoamuliwa na TFF isipokuwa kama ni dharura ya mvua au dharura yoyote nyingine basi mchezo huo utachezwa siku inayofuata iwapo ratiba inaruhusu
(e) Iwapo mchezo ulishaanza na kuvunjika kwa sababu ya mvua au dharura yoyote nyingine; magoli yaliyofungwa katika mchezo huo yataendelea kuwekwa katika idadi ya magoli yaliyofungwa na wachezaji binafsi lakini si katika idadi ya magoli ya timu. Kadhalika kadi walizoonyeshwa wachezaji katika mchezo ulioahirishwa au uliovunjika zitaendelea kuhesabika.
(f) Taarifa ya maombi ya kuahirisha mchezo ni lazima itolewe kwa maandishi si chini ya siku 14 kabla ya siku ya mchezo, isipokuwa kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa binadamu.

Katika kanuni hii, Sijaona kipengele kwamba mchezo unaweza kuahirishwa kwa sababu ya timu pinzani kunyimwa kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja husika.Tumeshuhudia michezo na figisu nyingi katika michezo ya CAF ikiwemo wachezaji kupuliziwa madawa katika vyumba vya kubadilishia, wachezaji kuvamiwa hotelini nk. Lakini haujawahi kusikia mchezo wa CAF umeahirishwa kwa sababu hizo, sanasana hatua huchukuliwa baada ya mchezo ila mchezo husika huachwa umalizike kwani kwa kusimamisha mchezo husika madhara ni makubwa zaidi.Je, nani atarejesha gharama za tiketi, malazi ya hoteli, wafanyabiashara mbalimbali waliowekeza kwa ajili ya mchezo tarehe husika?.Ni mara chache sana mchezo ukaahirishwa. Ninaamini pia sababu hizohizo ndizo zilipelekea mchezo kati ya Pamba na Simba kuruhusiwa kuchezwa licha ya kuwepo kasoro kadha wa kadha, Ndivyo hivyo mchezo wa JKT Queens ambapo bodi ya Ligi haikuamua kuhamisha mchezo huo tarehe nyingine bali ilitoa adhabu hapo hapo, na mchezo ulihesabiwa na JKT Queens waliadhibiwa vikali. Naamini sababu hizohizo ndizo zilizoiadhibu Biashara utd.

Kama mchezo unaweza kuahirishwa bila sababu ya msingi, na TPLB wakaona ni sawa, Itafika wakati timu ya ligi haitakuwa tayari kwa mchezo itatafuta sababu yoyote na Bodi itabariki kwa kusogeza tarehe mbele.

Hii inaondoa kabisa ile lengo la kanuni kwamba "Timu isipofika uwanjani, basi timu pinzani itapatiwa alama 3 na magoli 3. Sasa kanuni hii ina maana gani kama kuna uwezekano wa kukaa na kuyamaliza na mchezo ukapangwa wakati mwingine, Kanuni hii ina maana gani?

Bodi ya Ligi inapaswa kujitafakari sana. Ninyi ndiyo mnaotunga kanuni na nyie ndiyo wa kwanza kuvunja kanuni.
Wametumia busara kutoka juu huko kwenye system, ambazo zimesababisha bodi kwasasa Iwe na kigugumizi wanasubiri hiyo hiyo system itoe maelekezo baada ya kuchafua hali ya hewa, kikikiki

Kwakifupi bodi ya ligi hamna kitu wamedhihirisha kwamba wapo kama sanamu, (figure heads)
 
Back
Top Bottom