Atukuzwaye
Senior Member
- Oct 5, 2026
- 191
- 250
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imesema imerejesha utaratibu wa awali wa ununuaji wa tiketi wakati maboresho ya mfumo mpya yakiendelea kufanyiwa kazi.
“Simba dhidi ya Young Africans upo kwenye mfumo na mashabiki wanaweza kununua tiketi”
Kaimu Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Yahya Abushehe anasema kulikuwa kuna maboresho kwenye mfumo wa ununuzi wa tiketi ambapo hapo awali kulikuwa na uhitaji wa barua pepe (email) pamoja na watu wasio na vifaa (simu) vinavyotumia internet kushindwa kununua tiketi.
Soma: Simba yadaiwa kugomea Kampuni mpya ya Uuzaji Tiketi za Dabi ya Kariakoo
Kaimu Ofisa Habari wa TPLB, Abushehe, anasema wamebaini maboresho hayo yanaweza kuchukua muda mrefu na sasa wamesitisha na kurejea kwenye utaratibu wa awali. Abushehe amesema mchezo wa Dabi ya Kariakoo (Simba na Yanga) tayari umewekwa kwenye mfumo na mashabiki wanaweza kununua tiketi.