Bodi ya Ligi uso kwa uso na viongozi wa Yanga kujadili sakata la Derby ya Kariakoo

Bodi ya Ligi uso kwa uso na viongozi wa Yanga kujadili sakata la Derby ya Kariakoo

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Bodi ya ligi kuu tanzania bara TPLB imekutana na viongozi wa yanga Leo asubuhi kujadili hatma ya mchezo nambari 184 ulioahirishwa Tarehe 8 mwezi march mwaka huu kutokana na sababu ambazo Bado hazijawekwa wazi na Bodi hiyo.

Baadhi ya viongozi wa yanga waliohudhuria katika kikao hicho ni makamu mwenyekiti wa yanga Arfat haji , mkurugenzi mtendaji Adre mtime na afisa habari na mawasilino Ali Kamwe, kinachosubiriwa ni je? Viongozi wa yanga wataridhia kuchezwa Derby ya kariakooo.

Ikumbukwe kuwa baada ya mchezo kuahirishwa yanga walipeleka kesi ya kudai kupatiwa Alama 3 na magoli matatu kesi ambayo walishindwa baada ya jukumu la kesi hiyo kurudishwa katika mamlaka za ndani yaani TFF na TPLB, baada ya hukumu ya CAS Bodi ya ligi ikaupangia Tarehe mpya mchezo kati ya Yanga na Simba na yanga kutangaza rasmi kutokushiriki mchezo huo.

Soma Pia: Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mguto: Walio tengeneza Tisheti za 'Hatuchezi' hatuwaingilii ila dabi ipo!


Derby ya kariakooo imepangwa kuchezwa juni 15 katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar Es Salaam siku ya Jumamosi majira ya saa 11 jioni ingawa viiingilio vya mchezo huo havijatangazwa.


derby.png
 
Fukuto Linazidi kupanda.....!

Tunasubiri mapovu na matamko zaidi...!
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Bodi ya Ligi 🚮

Hawakuwa na sababu ya kuungana na ile timu iliyo kimbia mechi kwa kisingizio dhaifu chakuzuiliwa kufanya mazoezi siku moja kabla ya mchezo, as ilikuwa inatoka nje ya nchi! Kumbe ilitoka kuutumia uwanja huo huo kwenye mchezo mwingine, wiki moja tu iloyopita.
 
Maazio ya Utopwinyo ni ya kishambaa ati
Bodi ya ligi iachie ngazi yote ndo wacheze mechi - ha ha ha ha
 
Maazio ya Utopwinyo ni ya kishambaa ati
Bodi ya ligi iachie ngazi yote ndo wacheze mechi - ha ha ha ha
Hayo ni maazimio ya mashabiki Kwa mujibu wa makamu wa rais wa klabu hiyoo
 
Back
Top Bottom