Bodi ya ligi wangeweza kufuta matokeo badala ya kufuta mechi kama walihisi kuna rushwa.

Bodi ya ligi wangeweza kufuta matokeo badala ya kufuta mechi kama walihisi kuna rushwa.

Bodi ya ligi inahanyahanya iseme nini baada ya kuamrishwa na Simba ifute mechi ya derby. Kama takukuru ingethibitisha kuwa Yanga imetoa rushwa kwa yeyote ili kushinda mechi bado bodi ya ligi ingeweza kutumia ushahidi huo wa TAKUKURU kuipoka Yanga points 3 na kuipa Simba, lakini sio kuahirisha mechi masaa 3 kabla ya mechi kwa dhana na tetesi tu. Jeshi la polisi walisema walijipanga kikamilifu kwa mchezo wa derby tarehe 8 kudumisha usalama kabla, wakati na baada ya mechi, nani kasema derby isingekuwa salama? isingekuwa salama kwa nani, wachezaji, waamuzi, viongozi wa bodi au kwa mashabiki wa timu ipi? ni utetezi wa mfa maji tu. Maanda huwezi kuhukumu jambo kubwa kama lile ililiandaliwa kwa miezi mingi kwa kutumia tetesi na hisia masaa 3 kabla ya mechi; ni uhuni wa kishamba kabisa.

Baada ya Simba kufungwa magoli 5-1 na Yanga, simba waliwatuhumu akina Aishi Manula na wenzake kuwa walikula rushwa Simba ifungwe; mbona bodi ya ligi na TFF haikufanya uchunguzi wa tuhuma hizo nzito? Mwamuzi Smart alimpa red card mchezaji Mukombozi na kadi hiyo ikafutwa kuwa ilitolewa kinazi, mbona bodi ya ligi na TFF hawakufanya uchunguzi kwanini jambo lile lilitokea? Why derby?
Bodi ya ligi, polisi na takukuru imewakataa,toka jana wana kazi ya kupost mafanikio wanayoyaita ya karia,halafu mwenyekiti wake ndio kajichanganya kabisa
 
Bodi ya ligi imevuliwa nguo na Simba. Bodi iliahirisha mechi kwasababu Simba walisema hawapeleki timu.
Bodi imefafanua sababu za kuahirisha mechi. Hakuna mahali walipotaja kuwa sababu mojawapo ni Simba kusema hawapeleki timu.
 
Bodi ya ligi inasubiri kupewa hali ya majeruhi wa Simba camara na che malone ili wapange trh ya mechi kurudiwa, kwani hatujui?. Simba walikimbiziwa kucheza harakaharaka mechi zake na Fountain gates na Tabora United kabla hizo timu hazijakamilisha usajili wa wachezaji wake muhimu ili wapate matokeo kwennye mzunguuko wa kwanza. Mungu huyu hachezewi wala kudhihakiwa; 5imba watafungwa tena hata wakisogeza mechi wapi. Hakimu wa myonge ni Mungu.
Screenshot_20250319_180215_Threads.jpg

Hawa ndio wanaoongoza bodi ya ligi,mkuu ulitegemea nini unadhani GENTAMYCINE unaweza kukuta nae mjumbe hapo wa bodi ya ligi
 
Bodi ya ligi, polisi na takukuru imewakataa,toka jana wana kazi ya kupost mafanikio wanayoyaita ya karia,halafu mwenyekiti wake ndio kajichanganya kabisa
Anaongelea busara, hatutaki busara
 
Ingekuwa rahisi kuacha mechi ichezwe na kufuta matokeo kuliko kuahirisha mechi kwa sababu Simba imezuiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja ambao wanaufahamu. Busara ingekuwa bodi ya ligi kuacha mechi ichezwe kwenye uwanja ambao timu zote zinaujua.
 
Back
Top Bottom