Bodi ya ligi yasogeza michezo mbele kuipisha Yanga kimataifa

Bodi ya ligi yasogeza michezo mbele kuipisha Yanga kimataifa

Franky Samuel

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2018
Posts
5,195
Reaction score
13,785
Hapa bodi ya ligi na TFF mmefanya jambo la maana kwa maslai makubwa ya mpira wetu

===

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inawataarifu kuwa timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/2023 zitacheza michezo yao ya mwisho (mzunguko wa 30) Juni 9, 2023 ili kutoa nafasi kwa klabu ya Young Africans kucheza michezo yake miwili ya Fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika Mei 28 a Juni 3, 2023 dhidi ya klabu ya USM Algiers ya chini Algeria.

Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu ya NBC iliyotumwa kwa klabu hivi karibuni na kutangazwa kwa umma jana, michezo ya mwisho kwa klabu zote (ukiondoa Tanzania Prisons na Young Africans) ilipangwa kufanyika Mei 28, 2023 lakini Bodi imelazimika kufanya mabadiliko hayo baada ya majadiliano ya ndani yaliyojikita katika kuhakikisha uwepo wa haki na usawa michezoni kwa kuondoa mazingira yanayoweza kuchangia upangaji wa matokeo katika michezo hiyo.

Mabadiliko hayo yanakwenda sambamba na mabadiliko ya tarehe ya michezo ya munguko wa 29 ambapo sasa timu zote zitacheza Juni 6, 2023.

Bodi inatambua kuwa klabu zilianza kufanya maandalizi ya michezo hiyo kwa tarehe zilizotangazwa awali a kwa masikitiko inafahamu kuwa mabadiliko haya yanaweza kuathiri maandalizi hayo kwa namna moja ama nyingine. Hata hivyo, Bodi inapenda kufahamisha umma kuwa imelazimika kufanya mabadiliko hayo kwa maslahi mapana ya Ligi na mpira wetu kwa ujumla.

Bodi inazitakia klabu zote maandalizi mema ya michezo iliyosalia na kila la kheri katika kukamilisha msimu wa 2022/2023.

Imetolewa na;
Idara ya Habari a Mawasiliano
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
Mei 21, 2023

20230521_120305.jpg
 
Wengine wangemaliza mechi zao kwa jinsi ratiba ilivyo. Mechi ya leo ya Singida ingetakiwa kuchezwa kama mwanzo haikutakiwa kuahirishwa, kwa maana hiyo leo na Jumanne Yanga angekuwa anamaliza mechi zake za Mbeya halafu arudi Dar kusubiri kupigwa na mwarabu.
 
ukikaidi utapigwa2
unataka wapange matokeo? uliona wapi mechi za mwisho wa ligi zinazo husisha timu kushuka au kuchukua ubingwa zikachezwa mda tofauti?
 
unataka wapange matokeo? uliona wapi mechi za mwisho wa ligi zinazo husisha timu kushuka au kuchukua ubingwa zikachezwa mda tofauti?
Upangaji matokeo haufanyiki mechi za mwisho pekee. Tulipokuwa tunalalamika kuwa kwa karibu nusu msimu Simba amekuwa anacheza siku moja kabla ya Yanga, hamkuona uwezekano wa mmoja wao kufaidika na hiyo ratiba? Kwa nini kuelekea kwenye mbio za ubingwa mechi za Simba na Yanga hazikuwa zinapangwa kuchezwa muda mmoja?

Wachezaji wanauza mechi toka mwanzoni mwa ligi isitoshe wakati ligi inaenda kuisha?
 
Upangaji matokeo haufanyiki mechi za mwisho pekee. Tulipokuwa tunalalamika kuwa kwa karibu nusu msimu Simba amekuwa anacheza siku moja kabla ya Yanga, hamkuona uwezekano wa mmoja wao kufaidika na hiyo ratiba? Kwa nini kuelekea kwenye mbio za ubingwa mechi za Simba na Yanga hazikuwa zinapangwa kuchezwa muda mmoja?
Kuelekea kwenye ubingwa gani wakat yanga alikuacha points 8 mpk pale ulipomfunga zikapungua zikabaki 5
 
Huu ni ujinga wa kiwango cha 5G. Unaahirisha ligi nzima kwa sababu ya timu moja? Hizi gharama za ziada kwa timu nani anakwenda kuzibeba?
huu ni ujinga uliopitiliza. sasa wanavyosemaga kuwa wamezingatia mashindano yote mbona wanabadilisha ratiba. kweli sie kichwa cha mwendawazimu kila mmoja anajifunza kunyoa. alafu hao hao wanasema vilabu havina hela lakini maamuzi yananayofanywa yanakinzana na uhalisia
 
Ratiba ya mashindano makubwa lazima itaathiri mashinda madogo
NBC PL inabidi ipishe yanga ijiandae vyema ilete kombe nyumbani na taifa lipate heshima
 
Ratiba ya mashindano makubwa lazima itaathiri mashinda madogo
NBC PL inabidi ipishe yanga ijiandae vyema ilete kombe nyumbani na taifa lipate heshima
Kwani hizo tarehe za final zilikuwa hazijulikani before? Ishu ni kwamba wao wanashindwa kupanga mambo vizuri. Maana fifa caf dates zinajulikana mapema kabisa. Kuna timu zimekaa mieI miwili wanacheza mechi mbili sii ujinga huo
 
Mbona ligi kuu ya england nayo imesogezwa mbele kupisha fainali ya ligi ya mabingwa kwasababu city yupo fainali?

NIELEWE VEMA
 
Back
Top Bottom