Bodi ya Maji ya Uroki Bomang'ombe wilayani Hai yajenga Choo kipya baada ya uchakavu wa Choo cha wanafunzi katika Shule ya Msingi Kiselu

Bodi ya Maji ya Uroki Bomang'ombe wilayani Hai yajenga Choo kipya baada ya uchakavu wa Choo cha wanafunzi katika Shule ya Msingi Kiselu

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Uchakavu wa Choo cha wanafunzi katika Shule ya Msingi Kiselu iliyopo Kata ya Machame Uroki Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro uliyokuwa ukihatarisha usalama wa wananfunzi katika shule hiyo kutokana na choo hicho kuwa na dalili za kutitia umepatiwa ufumbuzi baada ya Bodi ya Maji ya Uroki Bomang'ombe wilayani humo kujitolea kwenda kujenga Choo kipya na chakisasa.

Meneja wa Uroki Bomang'ombe Mhandisi Arnold Mbaruku amesema kuwa wanatumia kiasi cha Shilingi Milioni 25 mpaka kukamilika kwa vyoo hivyo ikiwa nikama sehemu yakurejesha kwa Jamii na pia walichukua hatua hiyo kutokana na Shule hiyo kuwa Jirani na Chanzo kikubwa cha maji ya Uroki cha SAKI ambapo pia itasaidia kulinda mazingira ya Chanzo hicho.

Akizungumza leo Ijumaa March 7, 2025 baada yakutembelea shule hiyo Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafuwe amesema kuwa shule hiyo ilikuwa na changamoto ya choo chakavu kutokana na shule hiyo kuwa kuwa Kongwe kwani ilijengwa miaka ya 1970 huku akibainisha kuwa haikuwa ikapata huduma ya matengenezo ya mara kwa mara kutokana na sababu mbalimbali.

 
Back
Top Bottom