Tetesi: Bodi ya mikopo (HESLB) kuingia mtaani kusaka wanufaika wasiolipa deni lao

Duuh!
Kuna siku tulikaa kijiwe tukawa tunapiga hesabu kiasi ambacho bodi inadai kwenye hicho kijiwe tu ikawa kama milioni 60+ ambayo haiwezi kulipwa kirahisi labda wawe wanakata kwenye mikeka wanayoshinda na ni kitu kigumu mno.
 
Hio bodi ikubali tuu kua inajiendesha kihasara,
Wanufaika laki 2 na ushee kwa mwaka halafu ajira rasmi kwa mwaka ni kwenye elf 17,

Zaidi ya 700B Zingeingizwa kitaa chache ziende kwenye zile course zenye uhitaji kweli kweli ambapo wahitimu hawatakaa kitaa
 
Kuna taarifa za kwamba BODI ya MIKOPO inaanza kuingia mtaani.

Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu inataka kushirikiana na serikali za mitaa kuwatafuta watu wasio na ajira rasmi na walikuwa wanufaida wa mikopo ili iwadai pesa zao.

Mtu amemaliza Chuo kikuu hela ya vocha tu inamshinda ataweza kulipa deni la Mkopo?
Wasubirie tukila jackpot tutawalipa
 
Nchi kusomesha watu wake ni wajibu, ni uwekezaji wenye tija kuzalisha vijana walioelimika vyema kukabiliana na changamoto za nyakati ili kuiletea nchi maendeleo ya haraka...serikali waanzishe mfuko wa elimu ya juu ambao watu wote wakiwemo wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara watachangia kupitia tozo badala ya kuwadai hawa vijana pesa nyingi kwa mkupuo huku wengi wao ndo wameanza ajira au bado wanahangaika huku na kule.​
 
Kuna siku tulikaa kijiwe tukawa tunapiga hesabu kiasi ambacho bodi inadai kwenye hicho kijiwe tu ikawa kama milioni 60+ ambayo haiwezi kulipwa kirahisi labda wawe wanakata kwenye mikeka wanayoshinda na ni kitu kigumu mno.
😂😂😂
 
Kuna taarifa za kwamba BODI ya MIKOPO inaanza kuingia mtaani.

Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu inataka kushirikiana na serikali za mitaa kuwatafuta watu wasio na ajira rasmi na walikuwa wanufaida wa mikopo ili iwadai pesa zao.

Mtu amemaliza Chuo kikuu hela ya vocha tu inamshinda ataweza kulipa deni la Mkopo?
Mi nilimuachia kazi MAGU Kwa ishu izo izo,...unakuta kimshahara hicho hicho kikatwe bodi,Pension TRA,NHIF,Chama cha wafanyakazi,WCF,.etc.,..nikaona cha kufia nini?
 
Kuna taarifa za kwamba BODI ya MIKOPO inaanza kuingia mtaani.

Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu inataka kushirikiana na serikali za mitaa kuwatafuta watu wasio na ajira rasmi na walikuwa wanufaida wa mikopo ili iwadai pesa zao.

Mtu amemaliza Chuo kikuu hela ya vocha tu inamshinda ataweza kulipa deni la Mkopo?
Hivi mtu akitaka afahamu kiwango anachodaiwa anaangaliaje ??

Nakusudia mtu amemaliza chuo miaka kadhaa ishapita na hajawahi kulipa hata 100 mbovu
 
Nchi kusomesha watu wake ni wajibu, ni uwekezaji wenye tija kuzalisha vijana walioelimika vyema kukabiliana na changamoto za nyakati ili kuiletea nchi maendeleo ya haraka...serikali waanzishe mfuko wa elimu ya juu ambao watu wote wakiwemo wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara watachangia kupitia tozo badala ya kuwadai hawa vijana pesa nyingi kwa mkupuo huku wengi wao ndo wameanza ajira au bado wanahangaika huku na kule.​
Hapo umenena mkuu, waweke hata asilimia kwa miamala ya pesa, au bidhaa Fulani inayogusa kila mwananchi ili watu wasome bure. Inakuwaje serikali ifanye biashara za mikopo yenye riba!
Yaani mie hiyo pesa sitokaa nilipe milele.
 
Hivi mtu akitaka afahamu kiwango anachodaiwa anaangaliaje ??

Nakusudia mtu amemaliza chuo miaka kadhaa ishapita na hajawahi kulipa hata 100 mbovu
Utaratibu nadhani unaenda ofisini ya Kanda uliyopo, unatoa details zako then wanakuangalizia.
ANGALIZO: Ukienda uwe umejipanga kulipa maana ndio unajitoa mafichoni hivyo.
 
Kuna taarifa za kwamba BODI ya MIKOPO inaanza kuingia mtaani.

Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu inataka kushirikiana na serikali za mitaa kuwatafuta watu wasio na ajira rasmi na walikuwa wanufaida wa mikopo ili iwadai pesa zao.

Mtu amemaliza Chuo kikuu hela ya vocha tu inamshinda ataweza kulipa deni la Mkopo?
waje wachukue hewa majumbani mwetu kwani wengine sasa tunaingia mwaka wa saba bila ajira
 
Back
Top Bottom