Bodi ya Mikopo(HESLB) kwanini mnawakata Watumishi wapya tofauti na utaratibu?

Bodi ya Mikopo(HESLB) kwanini mnawakata Watumishi wapya tofauti na utaratibu?

Zekoddo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
1,859
Reaction score
4,539
Wakuu habari za wakati,

Iko hivi, kipindi cha maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwenye mkataba ulisema kuwa HESLB wataanza kumkata mkopaji baada ya miezi 24 toka tarehe ya kuhitimu kwake mafunzo, iwe ameajiriwa ama amejiajiri.

Sasa kinachoshangaza HESLB wameanza kukata pesa kwa vijana walioajiriwa na diploma hali ya kuwa hata vyeti vya degree hawajapata na wala hawajawasilisha kwa waajiri wao. Ikumbukwe vijana waliomba mikopo ili waweze kusoma elimu ya juu na inabidi wakatwe pesa kutokana na matunda ya level hiyo ya elimu yaliombea mikopo.

Hii inashangaza sana.
 
Wakuu habari za wakati..!!
Iko hivi, kipindi cha maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwenye mkataba ulisema kuwa HESLB wataanza kumkata mkopaji baada ya miezi 24 Toka tarehe ya kuhitimu kwake mafunzo, iwe ameajiriwa ama amejiajiri...
Kwani yeye alishakopeshwa?
 
Vicious cycle, utumishi wa umma ni kazi za watoto wa masikini, bodi ya mikopo ipo kwa ajili ya kuhakikisha watoto wa masikini wanaendelea kuwa masikini wao na vizazi vyao na utajiri wao uishie kujenga nyumba ya kuishi na gari la kutembelea. Ukweli mchungu!
 
Unaweza ukawa sahihi
 
Aisee ukiingia tu ajirani miezi minne mingi wanaanza kuchukua Chao na hiyoo ni lazima maana maafisa utumishi ni Moja ya kazi yao kukuingiza kwenye makato hayo
 
Back
Top Bottom