Bodi ya Mikopo HESLB mbona kimya?

Bodi ya Mikopo HESLB mbona kimya?

Trubarg

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2020
Posts
4,388
Reaction score
7,223
Mei mosi Mheshimiwa Raisi alisema kwamba wanaondoa retension fee kwenye mikopo ya vyuo vikuu.. Kwa akili yangu ndogo nilitegemea bodi ya mikopo ingetoa mwongozo wa kipi kinafuata kam taasisi zingine zinavyofanya pale wanapopewa muongozo na viongozi wao..
Kinyume naoma mwezi wa pili huu unaenda watu wapo kimya..hiki ni kiburi au ni nini?
 
Kimya Kina Mshindo
Hapo Utakuta Wameshashindwa Kujiendesha
Wanajiuliza Nitoke Vp
 
Wamekaa kimya kama hawapo..
 
Yaani na kuna mdau alienda kuomba statement ya deni wakasema hawatoi.
 
Mwaka wa serikali unaanza tarehe 1 mwezi wa saba. For now, nothing can happen.
 
Walisema pia kwamba, wataweka mfumo ambapo mdaiwa anaweza kulitazama deni lake kupitia simu ya mkononi, lakini mpaka leo kimyaaaa!

Pia, ile sheria ya retention fees ilitungwa na bunge mwaka 2013, je, rais anaweza kuibadilisha sheria bila kupitia bungeni tena?

Wengine wanasema tamko la rais ni sheria! je, ni kweli? kama ni kweli, hao bodi waharakishe mchakato wa kuondoa retention fee na kumpa mdaiwa deni lake halisi.

Tutakuwa nao tena July, waache wajisahaulishe tu! July ni karibu sana.
 
Ikifika July itabidi wadaiwa wote tuanzishe kampeni ili agizo la rais litekelezwe.

Tatizo Tanzania kiongozi akitoa maagizo bila kutuatilia, watendaji nao hukaa kimyaa. Watendaji wamezoea kwamba, Watanzania huwa tunasahau, ila hili la bodi wadaiwa hatutasahu. Ikifika July lazima tuanze kampeni ya kufuatilia hili jambo kwa kweli!
 
Mei mosi Mheshimiwa Raisi alisema kwamba wanaondoa retension fee kwenye mikopo ya vyuo vikuu.. Kwa akili yangu ndogo nilitegemea bodi ya mikopo ingetoa mwongozo wa kipi kinafuata kam taasisi zingine zinavyofanya pale wanapopewa muongozo na viongozi wao..
Kinyume naoma mwezi wa pili huu unaenda watu wapo kimya..hiki ni kiburi au ni nini?
Kwani July imeshafika mkuu?
 
Waziri wa Elimu alishalitolea maelezo,utekelezaji wake unaanza July
 
Hv nyie mnaolalamika retention fee sijui mikopo huwa mnakatwa pesa ngapi, Na pesa hyo isiyoisha miaka yote ni pesa ngapi.. Kwanza nyie mliosoma zamani mnaweza kudaiwa zaid ya milioni 10..?
Shida iko kwa vijana wa sasa bhana, vyuo vina ada kubwa na boom liko juu.. Yaan ile MTU anamaliza tu chuo M20+ anadaiwa.. Bado hzo 15% zao plus ugumu wa ajira kama huu.. Acheni kelele na kulialia lipeni pesa za watu umma hizo.
 
Mm nilikopeshwa milioni 10 now nadaiwa milioni 19 die to hio retention fee..
 
Mei mosi Mheshimiwa Raisi alisema kwamba wanaondoa retension fee kwenye mikopo ya vyuo vikuu.. Kwa akili yangu ndogo nilitegemea bodi ya mikopo ingetoa mwongozo wa kipi kinafuata kam taasisi zingine zinavyofanya pale wanapopewa muongozo na viongozi wao..
Kinyume naoma mwezi wa pili huu unaenda watu wapo kimya..hiki ni kiburi au ni nini?
Wajinga na Wazembe sana hao. Mimi wananikata pesa mara mbili nilishawatumia email message huu mwezi wa tano (5) hawajajibu chochote

Halafu kuna miezi wamenikata pesa ila kwenye loan statement haioneshi kuwa wamenikata, hivyo wameiba pesa ya miezi mitatu.

Wezi wakubwa hawa HESLB.

Kama hawajibu message za watumishi wala za kutoka Zone Office wana kazi gani sasa, si watumbuliwe tu?
 
Walisema pia kwamba, wataweka mfumo ambapo mdaiwa anaweza kulitazama deni lake kupitia simu ya mkononi, lakini mpaka leo kimyaaaa!

Pia, ile sheria ya retention fees ilitungwa na bunge mwaka 2013, je, rais anaweza kuibadilisha sheria bila kupitia bungeni tena?

Wengine wanasema tamko la rais ni sheria! je, ni kweli? kama ni kweli, hao bodi waharakishe mchakato wa kuondoa retention fee na kumpa mdaiwa deni lake halisi.

Tutakuwa nao tena July, waache wajisahaulishe tu! July ni karibu sana.
Tamko la Rais lilisema hili suala ni mpaka Julai? au ni Immediate case?
 
Wajinga na Wazembe sana hao. Mimi wananikata pesa mara mbili nilishawatumia email message huu mwezi wa tano (5) hawajajibu chochote

Halafu kuna miezi wamenikata pesa ila kwenye loan statement haioneshi kuwa wamenikata, hivyo wameiba pesa ya miezi mitatu.

Wezi wakubwa hawa HESLB.

Kama hawajibu message za watumishi wala za kutoka Zone Office wana kazi gani sasa, si watumbuliwe tu?
Katika mazingira hayo kuna uwezekano makato mengine yananeemesha familia zao. Ila we subiri tu. Kuna mtu alitegemea juzi PM atarara mbele na wale wababe wa Kujilipa maposho?Iko siku hata bodi watakuja kuzitapika tu
 
Back
Top Bottom