Bodi ya Mikopo HESLB waanza kuwakata watumishi wa TGTS B kabla hawajabadilishiwa muundo wa utumishi

Bodi ya Mikopo HESLB waanza kuwakata watumishi wa TGTS B kabla hawajabadilishiwa muundo wa utumishi

Kama ndio hivyo hii hatari mkuu, waibadilishe hii sheria mara moja.Ni sheri kandamizi.
Sheria inataka mtumishi akikatwa makato yote abakiwe na fedha isiyopungua 1/3 ya mshahara wake. Ikiwa na maana huyo ticha akikatwa piga ua anatakiwa achiwe 143,000. Hivyo mshahara wake unaweza kukatwa hadi asilimia 66 lakini asilimia 33 aachiwe mwenyewe.
 
Lakin kama alikua na kazi tayari kwanini aliamua kukopa tena Heslb..ni heri angejibana kujisomesha kwa mshahara wake
 
Huyo mkurugenzi wa helsb inapaswa mama amsaidie maana inaonekana ameshindwa
 
Kama ni tatizo la Makato kwa watumishi wote sawa. Lakini kama hoja ni Kutetea TGTS B asikatwe 15% sijakuelewa.
Mathematically 15% ya Salary Scale Effect yake ipo pale pale hata kama utapata TGTS G au H
Kwa sababu the more you Earn the More 15% deduction...
 
Sheria inataka mtumishi akikatwa makato yote abakiwe na fedha isiyopungua 1/3 ya mshahara wake. Ikiwa na maana huyo ticha akikatwa piga ua anatakiwa achiwe 143,000. Hivyo mshahara wake unaweza kukatwa hadi asilimia 66 lakini asilimia 33 aachiwe mwenyewe.
Sheria kandamizi
 
Kuna sheria pia makato ya mtumishi yasizidi moja ya tatu ya mshahara wake.Asilimia kumi na tano ni ukiukwaji wa sheria
Hiyo ishu HELSB hawajali kabisa hata kama utabaki na 75k haiwahusu...wana roho mbaya sana
 
Mbona umeficha tarakimu...za hela ya heslb...tutajuaaje yaaani....labda ipo 0.00! Ebu imarisha ushahidi.
 
Hivi kukopa ukope wewe upewe hela.wakati wakulipa mkopo uje kulalamika huku na wajinga wachache wanaunga mkono huu ujinga
 
Kuna sheria pia makato ya mtumishi yasizidi moja ya tatu ya mshahara wake.Asilimia kumi na tano ni ukiukwaji wa sheria
Sasa alaumiwe Bodi au we mwenyewe? Watu mnakimbilia kukopa wenyewe huko bayport alafu mnataka bodi ndiyo isikate hela yake kisa tu wawaachie byport

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikumbukwe kwamba mtumishi ngazi ya cheti anaanza na TGTS B, akijiendeleza akapata shahada anatakiwa kubadilishiwa muundo na kufikia TGTS D ambayo ni mshahara ngazi ya degree.

Kwa wale waliojiendeleza wakati wa awamu ya tano (certificate na diploma) na wameshamaliza shahada zao na wakati wa masomo wakabahatika kupata mkopo wa HESLB, sasa asilimia 15% ya makato inawahusu bila kujali wapo daraja gani au wana mikopo mingapi ama wanaishi kwa ⅓ ya basic yao.

Ama kweli kula kulipa.
View attachment 1763968
Tatizo umasikini wetu unakua mzigo kwetu Yani nikikaa nawaza Sana kwa nini niliombaga huo mkopo jibu linakuja Ni sababu ya umasikini.Napambana Sana wanangu wasije Soma kwa kutumia mikopo hiyo ya Heslb
slide_1.jpg
 
Ikumbukwe kwamba mtumishi ngazi ya cheti anaanza na TGTS B, akijiendeleza akapata shahada anatakiwa kubadilishiwa muundo na kufikia TGTS D ambayo ni mshahara ngazi ya degree.

Kwa wale waliojiendeleza wakati wa awamu ya tano (certificate na diploma) na wameshamaliza shahada zao na wakati wa masomo wakabahatika kupata mkopo wa HESLB, sasa asilimia 15% ya makato inawahusu bila kujali wapo daraja gani au wana mikopo mingapi ama wanaishi kwa ⅓ ya basic yao.

Ama kweli kula kulipa.
View attachment 1763968
Maisha magumu sana
 
Back
Top Bottom