Bodi ya Mikopo hiki mlichotufanyia continuous ni nini?

300k kwa mwezi!! Ila maisha haya, na kuna mlinzi mahali analipwa 150k kwa mwezi na ana familia na anatoboa daah!!!
Hiyo 600000 ni geresha tu baada ya kulipa ada hapo hata 300k haubaki nayo
 
Naam Mkuu hapa umenena vyema kabisa na hii ndiyo HALI HALISI
 
Mimi huwa nashangaa sana kwa BODI kuamua kuwapa mkopo zaidi wasio na uwezo wa kulipa ada huku wakijua kuwa walewale ndiyo hawana uwezo wa kulipa hiyo mikopo. Hiki kigezo siyo sawa hata kidogo. Baadaye BODI inalalamika eti waliopewa mikopo hawarudishi ili na wengine wapewe wakati sababu kubwa ya kutorudishwa mikopo wanaijua. Hii akili ya wapi sijui. Financial illiteracy!
 
Pesa yenyewe mna fanyia uzinzi tu afu chuo kikiisha mna lia lia ajira pimbi nyie .mngesoma bila mkopo kama sisi mngeweza nyie
 
Iyo ada wazazi wanakusaidia kulipa ama ?? Ni kwenye hiyo 600k
 
Haya ni Maajabu
 
Umeandika madudu
Sasa hawana uwezo wa kuulipa kabla ya kupata kazi au baada ya kupata kazi?
Uwezo wa kuulipa unapima na nini ?
Kila mkopo una sheria zake.
 
Pesa yenyewe mna fanyia uzinzi tu afu chuo kikiisha mna lia lia ajira pimbi nyie .mngesoma bila mkopo kama sisi mngeweza nyie
Pesa ipi ya kufanyia uzinzi? Asilimia kubwa ya wanufaika hiyo pesa ya meals and accommodation inaishia kwenye ada tu
 
Umeandika madudu
Sasa hawana uwezo wa kuulipa kabla ya kupata kazi au baada ya kupata kazi?
Uwezo wa kuulipa unapima na nini ?
Kila mkopo una sheria zake.
Kwani kuwa na uwezo wa kulipa mkopo wa BODI YA MIKOPO kwa anayeomba mkopo siyo kigezo kimojawapo cha kutoa huo mkopo? Labda hapo unieleweshe nielewe!
 
Naomba kuuliza mfano mtu kapata 80% ya mkopo na ada ya huyo mtoto ni 1365000/= hapo SUA ina maana mm ka mzazi au mlezi huyo mtoto nitamchangia kiasi gani kwenye iyo ada na hela ya kula iyo elfu 10 anakuwa anapewa mm sihusiki tena hata akiwa likizo anapewa iyo elfu 10 nauliza ili nipate kujua wengine hatujafika chuo tusije pigwa na hawa vijana wa gen Z
 
Kwani kuwa na uwezo wa kulipa mkopo wa BODI YA MIKOPO kwa anayeomba mkopo siyo kigezo kimojawapo cha kutoa huo mkopo? Labda hapo unieleweshe nielewe!
Hapana kulipa ama kutokulipa ni matokeo tuu
Kwa sababu mtu anaweza kuwa na uwezo wa kulipa na asilipe .
Kigezo kilichopo ni cha mdhamini na sio awe na uwezo wa kulipa ama kutukulipa.
 
Ungeweka figure sahihi ya ada aliyolipiwa na serikali ingekuwa vyema

Ila nadhani hapo atakuwa kalipiwa kiasi cha 1,030,000 so kiasi kilichobaki ndo utahusika nacho mzazi

Hiyo elfu 10 ya meals and accommodation atapewa kila baada ya siku 60 atakazokuwepo chuoni kipindi cha likizo hawezi kupata imehesabiwa kwa mda atakaokuwepo chuoni tu
 
Hapo nmeelewa ss mkuu
 
Hapana kulipa ama kutokulipa ni matokeo tuu
Kwa sababu mtu anaweza kuwa na uwezo wa kulipa na asilipe .
Kigezo kilichopo ni cha mdhamini na sio awe na uwezo wa kulipa ama kutukulipa.
Anayeangaliwa kuwa na uwezo wa kulipa ni mdhamini siyo mwanafunzi. Au unaongelea jambo tofauti?

Kwa hiyo mdhamini kuwa na uwezo wa kulipa siyo kigezo kwa sababu anaweza akawa na uwezo wa kulipa na asilipe. Usibahatishe brother! Mimi naongelea kigezo kimojawapo kinachotakiwa kufuatwa wakati wa kutoa mikopo ili kuwa na uhakika wa kukusanya hiyo mikopo wakati unapowadia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…