Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,262
Ukweli ni kuwa hii tasisi ni kero kubwa kwa wanafunzi kutokana na usumbufu wanaopata wanafunzi na wazazi. Wanafunzi walishajaza maombi lakini Bodi sasa imeanza kuleta masharti kama mganga wa kienyeji mara wanafunzi wanaambiwa walege nyaraka zile zile ambazo washaziwasilisha kwaajili ya mikopo kwa kile wanachokiita kukata rufaa.
Rais alisha tamka hakuna mwanafunzi atakaye kosa mikopo lakini hali ilivyo sivyo hata wale wanafunzi waliowekewa vipaumbele kwa maana ya wasichana wanaosoma sayansi sasa nao wananyimwa mikopo. Mwanafunzi anapoambiwa akate rufaa wakati yupo nje ya chuo na wakati huo huo wenzake wanaendelea na masomo ni dhambi kubwa na kumpotezea muda. Rufaa yenyewe inatakiwa ithibitishwe na chuo na wakati huo huo chuo wanakataa kuthibisha kwakuwa mwanafunzi ili asajiliwe lazima alipe nusu ya ada. Mimi naona sehemu ambapo rais anapaswa sasa kuingia na kuwafutilia mbali viongozi ni hapo bodi ya mikopo.
Kusema wanafunzi wakate rufaa maana yake pesa ipo isipokuwa nao wanataka kujimwambafai kwa kuongeza urasimu. Watu washaomba mikopo halafu wanaambiwa wakate rufaa kana kwamba walikuwa na kesi wakashindwa. Mimi namuomba rais hebu aende pale loan board kwa ghafla na kuwatimua wote pale waende waka kae na wake zao nyumbani wanasumbua sana wanafunzi. Haiwezekani rais anasema pesa zipo na nchi hii ni tajiri halafu wanatokea wa kumkwamisha ili aonekane ni mwongo. Loan board kwakweli ni shida sana kwa wanafunzi.