Bodi ya Mikopo ongezeni tozo walau ifike 20%

KUMBUKA kuna watoto wa wanyonge toka huko ikungi hawana hata mlo na hawapati mkopo kabisa , kwanini tusigawane umaskini? laakini pia tumeona NCH yetu imeingizwa kwenye uchumi wa kati,

Mkuu shule ya msingi uliishia darasa la ngapi?

Mbona unajadili mambo ambayo yapo nje ya uelewa wako ujionea huruma na haibu?
 
Sasa hivi tunalipa 8% ambayo ni ndogo sana, walau wapandishe ifike 20% ili wadogo zetu na watoto wapate mkopo.
Ww sio mnufaika wa HESLB hata hujui wanakata kiasi gani? Eti 8% wakati wanakata 15%. Rudi shule tena
 
Mkuu msamehe huyo ni mbeba box pale lumumba
 

Ajira si lazma ujiajiri, hapa Mwanza kitangiri watu wanachemsha mayai wanauza, wanafunga maji ya kandoro wanauza, wanafanya kupaka watu rangi za kucha, wewe unataka upewe ofis, gari, AC na mke ndio useme ni ajira,? Vyuoni sijui mlifunzwa nini walah1

Hizo ajira ambazo kipato chake hakitabiliki watakataje hyo asilimia unayosema
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] umekunywa nini mkuu
Vijana wengi hawana ajira wako mtaani unadhani kuna mtu anapenda kudaiwa
Shukuru Mungu umepata kwa kujishikiza na ufanye utafiti darasani kwenu tangu umalize wangapi wamepata sehemu ya kujiingizia kipato usiropoke tu sababu we umeshiba hujui mwenye njaa
 
Tatizo siyo kukatwa asilimia 15 au 20 n.k ila ni kabla ya kukatwa unakuwa katika hali gani?...kuna watumishi wahishamaliza kiwango cha kukopesheka na hivyo kubaki na kiasi kinachowasustain tu, tabu inaongia pale makato ya "heslb" yananapokuwa huru kiasi cha kutozingatia kiasi a anachopaswa kubaki nacho mfanyakazi.
 
Ndiyo, wanakwambia lipa only 8% si inakatwa juu kwa juu kwenye mshahara? Wengi wetu tunataka wakate 20%

Wengi wenu na nani hasa mnaotaka mkatwe hiyo 20%?

Watoto wa mama huwa hamjifichi kabisa! Ungekuwa ni kijana mwenye majukumu usingeandika huu ushuzi wako.
 
Ndugu Victor umeongea kisomi na kwa hoja, ila wakati wa kuchukua mkopo huyo mtu alisaini na kukubaliana na terms, na anajua mwenye mamlaka ya ku-adjust marejesho ni HESLB, sasa hii ni tabia mbaya ya Watanzania, wakati wa kuomba mkopo anatoa mpaka machozi, akiupata anagoma kulipa.
 

Mimi nadhani kwako iwe 100% kabisa maana unataka sifa sasa
 
Wengi wenu na nani hasa mnaotaka mkatwe hiyo 20%?
Wanufaika wa HESLB na wazalendo, wanaokataa ni wahujumu uchumi na wasiopenda afanyacho MAGUFULI, in short ni watu wanaotumiwa kumkwamisha MAGUFULI.
 
Msisahau kiongeza na ajira na mishahara walau kwa 90%
 
Ndugu jaji mfawidhi kumbuka mkopo wa loan board ulizalisha masharti mapya ambayo hayakuwepo kwenye mkataba wa awali.
 
8% unalipa wewe na nani?? itakua hata ulichokiandika hukielew, walau ungepita hata kwenye publications usome ndo uje kuandka
 
Ndugu jaji mfawidhi kumbuka mkopo wa loan board ulizalisha masharti mapya ambayo hayakuwepo kwenye mkataba wa awali.
Moja wapo ya masharti ya mkataba wa awali ni kwamba "at any time watakapo ona inafaa, wata adjust marejesho, tatizo mlisaini bila kusoma kote, sisi pia huwa tunawasaidia watu kesi mahakamani, wanachukua mkopo CRDB, masharti yapo kwa maandishi madogo, mengi kurassa 10, mtu anakwambia hayana maana , anasaini, siku akishindwa kulipa ndio anakuja mahakamani ku plea "non eest factum' yaani SIKUJUA.
 
Acha kimbelembele au kwasababu wewe unaishi kwa shemeji.
Tuwe wazalendo na siyo kimbelembele, tupo kwenye vita ya kiuchumi na maadui wapo ndani na nje, wa ndani ni pamoja na wakopaji wasiotaka kurejesha mikopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…