Bodi ya Mikopo ongezeni tozo walau ifike 20%

Mlevi huyo kasikia watu wanajadili huko bar hakusikia vizuri alikuwa kalewa. Eti imeanzishwa 2005!

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hawa wanufaika ni watu hatari sana. Hawana mpango wa kulipa hizi pesa na wanasema wazi wazi kwamba hawalipi. Hii kazi ya kuwasaka na kuwatia adabu ipatiwe JWTZ. anapokamatwa mnufaika ambaye amekwepa kwanza aende national service mwaka mzima akajifunze uzalendo. Akitoka huko tuteue gereza maalum kwa ajili yao tuu huko ni kazingumu kwa miaka 10. Ndugu zake wakitaka atoke wamdhamini kwa maandishi na hiyo pesa iwe imrejeshwa ndani ya miaka 4. Wajinga sana hawa kuna mmoja nilimlipia sasa ni wakili namwomba anirejeshee hiyo pesa hata kidogo kidogo 20% ya mshahara wake. Jibu alilonipa ni kwamba kwani una shida ya pesa wewe?. Nimekuzulumu na ukitaka nenda mhakamani. Mimi ni wakili tutapambana huko huko. Sasa hata hao wa bodi wana kibri kama hiki cha mdeni wangu. Kazi kwenu mnaohusika na kudai hayo madeni. Mimi huyu ninaemdai namvutia pumzi nipate muda wa kushughulika naye lakini pesa yangu lazima ilipwe.
 
Bwana wakili Ngararimo naona unajua ubalisia wa hii kitu lakini una uzalendo kama wa MAGUFULI.
Hawa wanafaika wapo mitaani wanatamba kwamba hawarudishi huku wakiwabeza waliolipiwa fedha na wazazi wao.
Mawakili wengi walisoma kwa mkopo kwakuwa walikuwa na ufaulu wa alama A menas divisiona one mpaka three , ukiacha waliosoma Tumaini-chuo cha kata by then.
Watu waliowadhamini wawataje wanufaika, wanawajua,
 
Kwanza hakuna anayelipa 8%. Wote tunapigwa 15% wakati tuliingia contract ya 8%
Kuna wengine bado wanalipa 8% badala ya 15% nawafahamu kabisa, ndo ujue kuwa bodi ya mikopo hawapo serious na kazi yao japo Serikali inawabeba!
 
Wewe utakuwa agent wa shetani sio bure
 
20% mbona ndogo, wakate 100% kabisa ya mshahara. Hivi jwtz, polisi, tiss na wao wanakatwa au ni sisi 'walimu' na 'watendaji'?
 
Asilimia 15 unaiona ndogo? Kweli akili za kuambiwa Changanya na za kwako
 
Sasa hivi tunalipa 8% ambayo ni ndogo sana, walau wapandishe ifike 20% ili wadogo zetu na watoto wapate mkopo.
Kwani hivi sasa hao wadogo zenu na watoto wanakosa hiyo mikopo?
 
Kwani hivi sasa hao wadogo zenu na watoto wanakosa hiyo mikopo?
ndiyo, asilimia 60 ya wanao omba wanakosa, na wanaopata wanapata kwa madaraja , yaani wengi wanapata 60%,
 
20% mbona ndogo, wakate 100% kabisa ya mshahara. Hivi jwtz, polisi, tiss na wao wanakatwa au ni sisi 'walimu' na 'watendaji'?
Wote waliopo SErikalini wanakatwa, kwanini unataka Jeshi na TISS wakatwe wakati wao ndio walistahili kusamehewa maana hata majukumu yao ni mazito?
 
Sasa hivi tunalipa 8% ambayo ni ndogo sana, walau wapandishe ifike 20% ili wadogo zetu na watoto wapate mkopo.
Hujui chochote wewe, watu tunakatwa asilimia 15 na unataka tukatwe asilimia 20 kwa mshahara UPI?
 
Hujui chochote wewe, watu tunakatwa asilimia 15 na unataka tukatwe asilimia 20 kwa mshahara UPI?
Mshahara huo huo, kwani umewahi kusikia mtu duniani kasema mshahara wake unatosha?

DAS/wanaacha wanataka ubunge!

Wakuu wa wilaya wameacha wanataka ubunge
Wakuu wa mikoa[milioni 7] wanataka ubunge [milioni 12]!

Profesa mstaafu udsm anaacha wajukuu anataka ubunge!
wote hawa wanaona kiinua mgongo cha milioni 200 hakitoshi napia wanataka hela zaidi na ukimpigia simu anakwambia hana hela kabisa!

Mama zetu wanafagia barabarani na wanalipwa haifiki 200,000 na wanalipa deni!
Wewe upo halmashauri, hutaki kulipa? who are you?
 
Waongezewe hadi ifike asilimia 20,labda akili itawasogea na wapate ufahamu/wajitambue.
 
Only Great Thinkers will understand you.

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
nimeweka na klip ili waelewe. wakishindwa namuachia Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…