carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imefungua dirisha la rufaa kwa mwaka wa masomo 2026/2027 kwa muda wa siku saba, kuanzia Oktoba 25 hadi Oktoba 31, 2026.
Hatua hiyo inalenga kuwapa fursa wanafunzi wenye taarifa za ziada zinazoweza kuwawezesha kupata mikopo ya elimu ya juu kuwasilisha rufaa zao.
Katika taarifa kwa umma iliyotolewa Oktoba 25, 2026, HESLB imewahimiza wanafunzi kutumia muda uliopangwa kuwasilisha rufaa zao kupitia utaratibu uliowekwa na bodi hiyo.
HESLB imewataka wanafunzi kuhakikisha wanawasilisha rufaa zao ndani ya muda uliotangazwa ili kunufaika na fursa hiyo.