Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Mwanachama wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa Jukwaa la Elimu (Education Forum) aliandika “Kipengele kipya cha Anuani ya Makazi (NaPA) katika Fomu ya Mkopo wa HESLB hakieleweki kwa Watendaji wengi, HESLB itoe elimu”
Mwanachama huyo alidai kuwa uombaji wa mkopo wa Chuo kuna kipengele kipya cha kuweka National Physical Address (NaPA) ambacho kimekuwa kikwazo kwa waombaji wengi kutokana na kutokuwa na uelewa wa kipi cha kujaza.
Alichoandika Mdau ~ Kipengele kipya cha Anuani ya Makazi (NaPA) katika Fomu ya Mkopo wa HESLB hakieleweki kwa Watendaji wengi, HESLB itoe elimu
UFAFANUZI WA BODI YA MIKOPO...
Meneja Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Veneranda Malima amefafanua kuhusu suala hilo kwa kusema:
“Mwanafunzi kama mtegemezi anatakiwa awe amesajiliwa chini ya Mzazi au Mlezi, sisi tunachohitaji ni “reference” namba anayopewa.
“Siyo kitu kigumu kama baadhi wanaosema, anuani hiyo ya makazi ni jamboa ambalo linahitajiwa na kila mtu sio Wanafunzi pekee, unapohitaji unaomba kupitia Kiongozi wako wa Mtaa au Mtendaji wa Mtaa au Kijiji.
“Hata kama wewe mhusika una nyumba 10 au zaidi, unatakiwa kuchagua moja ambayo umejisajili hasa eneo unaloishi na kuitumia.
“Wanafunzi wao tunawashauri wajisajili kupitia anuani za Wazazi wao au Walezi kwa kuwa ndio makazi yao yalipo.
“Pia, kila siku jioni HESLB kwa kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano tunatoa elimu kupitia njia ya Mtandaoni katika Google Meet, humo mtu anapata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali na anajibiwa, mbali na hapo elimu hiyo tunaitoa kupitia kurasa mbalimbali za Kijamii.”