Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Ukisikia bureaucracy ndio hii sasaMtu tayari una NIDA ambayo inataarifa zote na kabla ya kupata NIDA unapitia kwa hao viongozi wa mtaa, kwa nini taarifa za NIDA zisitumike huko NaPA
hiyo namba ya ufuatiliaji utaweka na utabonyeza hakuna majibu wengine wanawiki ya pili sasaMwanachama wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa Jukwaa la Elimu (Education Forum) aliandika “Kipengele kipya cha Anuani ya Makazi (NaPA) katika Fomu ya Mkopo wa HESLB hakieleweki kwa Watendaji wengi, HESLB itoe elimu”
Mwanachama huyo alidai kuwa uombaji wa mkopo wa Chuo kuna kipengele kipya cha kuweka National Physical Address (NaPA) ambacho kimekuwa kikwazo kwa waombaji wengi kutokana na kutokuwa na uelewa wa kipi cha kujaza.
Alichoandika Mdau ~ Kipengele kipya cha Anuani ya Makazi (NaPA) katika Fomu ya Mkopo wa HESLB hakieleweki kwa Watendaji wengi, HESLB itoe elimu
UFAFANUZI WA BODI YA MIKOPO...
Meneja Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Veneranda Malima amefafanua kuhusu suala hilo kwa kusema:
“Mwanafunzi kama mtegemezi anatakiwa awe amesajiliwa chini ya Mzazi au Mlezi, sisi tunachohitaji ni “reference” namba anayopewa.
“Siyo kitu kigumu kama baadhi wanaosema, anuani hiyo ya makazi ni jamboa ambalo linahitajiwa na kila mtu sio Wanafunzi pekee, unapohitaji unaomba kupitia Kiongozi wako wa Mtaa au Mtendaji wa Mtaa au Kijiji.
“Hata kama wewe mhusika una nyumba 10 au zaidi, unatakiwa kuchagua moja ambayo umejisajili hasa eneo unaloishi na kuitumia.
“Wanafunzi wao tunawashauri wajisajili kupitia anuani za Wazazi wao au Walezi kwa kuwa ndio makazi yao yalipo.
“Pia, kila siku jioni HESLB kwa kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano tunatoa elimu kupitia njia ya Mtandaoni katika Google Meet, humo mtu anapata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali na anajibiwa, mbali na hapo elimu hiyo tunaitoa kupitia kurasa mbalimbali za Kijamii.”
watendaji wanavyo ringa sasa mwanafunzi akienda atazungushwa weee kama ni wa kike ataambiwa rudi kesho mara kesho kutwa yote ni kumtengenezea mazingira flani. ila kama ni wa kiume ataambiwa nipo bize kama vip fanya mpango wa kifurushi/data na salio kidogo ya maisha. Yaani taabu tupu wengi watakwamaSasa kama suala limewekwa kidigital kwanini ipatikane kupita viongozi wa mtaa na kijiji tu...kwanini wasingewezesha mtu binafsi kuipata bila kupitia kwa hao viongozi?....Hili litakua ni kero sanaa.
Napa hawakujiandaa vizuri katika hiliwatendaji wanavyo ringa sasa mwanafunzi akienda atazungushwa weee kama ni wa kike ataambiwa rudi kesho mara kesho kutwa yote ni kumtengenezea mazingira flani. ila kama ni wa kiume ataambiwa nipo bize kama vip fanya mpango wa kifurushi/data na salio kidogo ya maisha. Yaani taabu tupu wengi watakwama
Tatizo ulisoma bila kutafakariMtu tayari una NIDA ambayo inataarifa zote na kabla ya kupata NIDA unapitia kwa hao viongozi wa mtaa, kwa nini taarifa za NIDA zisitumike huko NaPA
Muombe mwenye nyumba jina lake kamili na no. ya nyumba hapo mnaoishi, then wazazi wako na ww mtasajiliwa kama wapangaji wa huyo mwenye nyumba, then utaendelea na mchakato wako, Ila kama mwenye nyumba hajasajiliwa inabidi afanye hivyo halafu awasajili nyie kama wapangajiNaomba niulize kwa sisi ambao wazazi wetu wamepanga inakuwaje kuhusu NAPA, kusaidia Maombi ya mkopo
Mkuu msaada Mimi naanza kuomba niamzie wapiMuombe mwenye nyumba jina lake kamili na no. ya nyumba hapo mnaoishi, then wazazi wako na ww mtasajiliwa kama wapangaji wa huyo mwenye nyumba, then utaendelea na mchakato wako, Ila kama mwenye nyumba hajasajiliwa inabidi afanye hivyo halafu awasajili nyie kama wapangaji
Kwa mtendaji wa mtaa, wako,Mkuu msaada Mimi naanza kuomba niamzie wapi
MZAZI NA MTOTO WANAWEZA KU SHARE HIYO NaPA AU KILA ANAKUWA NA YA KWAKE ?Muombe mwenye nyumba jina lake kamili na no. ya nyumba hapo mnaoishi, then wazazi wako na ww mtasajiliwa kama wapangaji wa huyo mwenye nyumba, then utaendelea na mchakato wako, Ila kama mwenye nyumba hajasajiliwa inabidi afanye hivyo halafu awasajili nyie kama wapangaji