Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa Mwanafunzi na Mnufaika wa mikopo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kudai wamecheleweshewa fedha za kujikimu (Boom) kwa wiki mbili sasa, ufafanuzi umetolewa.
Hoja ya awali hii hapa ~ Bodi ya Mikopo ya Vyuo Vikuu (HESLB) inatuweka Wanachuo katika wakati mgumu sana kwa kutotuwekea fedha
Akifafanua jambo hilo la Mdau huyo aliyejitambulisha kuwa Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kampasi Kuu ya Mwalimu Nyerere, Veneranda Malima ambaye ni Meneja Mawasiliano wa HESLB amesema:
Tunapofanya malipo nasi pia tunakuw atunategemea baadhi ya Wadau wengine kadhaa ikiwemo benki, kulikuwa na changamoto ya mifumo ya Kibenki ambayo imechangia malipo kuchelewa
Tunatarajia kuwa kuanzia kesho waaanza kupata fedha hizo wanazostahili kuzipata na kama mifumo itakuwa sawa, kuna uwezekano hata leo (Mei 28, 2025) wanaweza kuanza kupokea baadhi yao.
Pia, tuwajulishe kuwa mchakato ukichelewa haimaanishi hawatalipwa, wale wote wanaostahili kulipwa na wamekamilisha nyaraka zote watalipwa.
Pamoja na hivyo Wanafunzi wanafahamu kuwa wanapopata changamoto za malipo jambo la kwanza wanatakiwa kuwasiliana na Afisa Mikopo katika Vyuo vyao kwa kuwa malipo yanahusisha mtu mmojammoja na yanahusisha mifumo ya kidigitali.
Yeyote mwenye changamoto anaporipoti kwa Afisa Mikopo anapata msaada wa kuelezwa nini cha kufanya.