Bodi ya mkopo elimu ya juu mwaka ujao nilipe tena?

Bodi ya mkopo elimu ya juu mwaka ujao nilipe tena?

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Kwenye gazeti la leo la Mwana Habari pana habari inayosemeka 'Rais Samia apeleka kicheko elimu ya juu'.
Habari hii inahusu mikopo kwa wanafunzi wa vyuo.
Kwa kweli nimefadhaika mno kwani niña binti ambae kateuliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salamm (UDSM) kwa mwaka wa kwanza.
Tarehe 4/09 nililipa sh30, 000/= kwenye bodi za Kuombeana mikopo na tarehe 6/09 nikalipa sh6, 000/= za kuhakiki cheti cha kuzaliwa.
Kilichosumbua ni kutumia kitambulisho changu tu ila taarifa nyengine zilitimwa.
Baada ya dirisha kufungwa, tulitumai kupata ujumbe wa kuthibitisha au kututaka kuboresha taarifa hizo. Mpaka sasa hakuna chochote na awamu ya tatu wamesema wataitangaza wakati wowote.
Mie ni mstaafu miaka minne iliyopata ni kikokotoo kilikuwa 25% ya kiinua mgongo hivo pamoja na mambo mengine nilimlipia binti masomo ya Chuo baada ya kugonga mwamba kwenye mkopo.
Nnachojiuliza, mwaka ujao nikimuombea mkopo binti ambae atakuwa nyumbani mwaka huu, itabidi kulipa tena gharama hizo?
 
Utalipia tena mkuu. Samahani, kwanini ulichelewa kumuombea mkopo hadi pale ilipofika dirisha la nyongeza?

Maana dirisha lilifunguliwa tangu June mosi hadi Agosti 31 ni kipindi cha miezi mitatu.

Ukiwahi kuomba mkopo mapema unakuwa kwenye position nzuri ya kufanya marekebisho (if any) lakini kuomba dakika za majeruhi mtandao huwa unasumbua.
 
June? Mbona matokeo ya kidato cha sita yalitoka July au!
 
Safi sana..nafurahi kusikia wastaafu wa umma mnateseka..sabb mnapokua kwenye hayo maofisi ya umma hamna huduma ya maana mnayotoa Zaid ya rushwa , kiburi, ujeuri na kupotezea wengine mda wao..

hyo ni Moja ya laana zitazokuandama mpaka unakufa!!am watching 🤣🤣
 
June? Mbona matokeo ya kidato cha sita yalitoka July au!
Dirisha lilifunguliwa June mosi. Nani alikwambia dirisha la mikopo linafunguliwa kwa kuangalia mitihani ya kidato cha sita pekee?

Kuna watu wa level mbalimbali wanahitaji mkopo kuanzia Law School, Masters, Waliotoka Diploma kwenda Degree nakadhalika.

Pia waombaji wa mikopo sio lazima wawe form six wa mwaka husika bali kuna form six wa miaka ya nyuma ambao wengine waliomba wakakosa na wengine walimaliza form six miaka ya nyuma ila hawakuomba mkopo hivyo ndiyo wanaomba kwa mara ya kwanza.
 
Oh! Shukran kwa kunielewesha mkuu.
 
Back
Top Bottom