Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), imegoma kuidhinisha mabilioni ya shilingi yaliyolenga kutumika kujenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Serengeti, mkoani Mara, MwanaHALISI limeelezwa.
Vyanzo vya taarifa kutoka wilayani Serengeti na makao makuu ya PSSSF jijini Dar es Salaam, zinaeleza kuwa bodi imegoma kuidhinisha matumizi ya mabilioni hayo ya shilingi, baada ya kujiridhisha kuwa ujenzi wa uwanja huo, "hauna manufaa kwa mfuko."
Mradi huo, unadaiwa kupigiwa chapuo kwa ustadi mkubwa na Rhimo Nyansaho, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF; na Fortunatus Magambo, mkurugenzi wa sasa wa mfuko.
Kwa sasa Nyansaho ni mbunge wa kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, na ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, mradi huo unatarajiwa kutumia zaidi ya Sh. 362.47 bilioni (sawa na dola za Marekani 144.98 milioni), kutoka kwenye mfuko wa akiba kwa watumishi wa umma.
"Bodi imejiridhisha kwamba mradi wa ujenzi wa Serengeti International Airport (SIA), hautakuwa na faida kibiashara. Uchambuzi yakinifu umeonesha mradi unakabiliwa na hatari 13 zenye kiwango cha juu na kwamba hakuna kokote ambako gharama za kukabiliana na hatari hizo kumeonyeshwa.
"Wala mradi hauoneshi jinsi wawekezaji watakavyoweza kulipwa fidia kwa kubeba hatari hizo," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Kuvuja kwa taarifa hizi, kumekuja wiki moja baada ya serikali kutangaza kuvunjwa kwa bodi ya wakurugenzi ya mfuko huo na hadi tunakwenda mitamboni Jumanne, bodi mpya ilikuwa bado haijateuliwa.
Bodi iliyovunjwa ilikuwa inaongozwa na Joyce Mapunjo, aliyekuwa Katibu Mkuu Hazina.
Soma Pia: Rais Samia avunja Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF)
Mapunjo aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa bodi ya PSSSF, tarehe 2 Desemba 2024, kuchukua nafasi ya Mhandisi Musa Iyombe.
Bodi ya Mapunjo ilizinduliwa 27 Machi 2025 na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete.
Wajumbe wengine wa bodi walikuwa Pius Maneno (makamu mwenyekiti), Bi. Emma Lyimo, Dk. Haphsa Hincha, Tumaini Nyamhokya, Suzanne Doran, Vicky Jengo na Sadi Shemliwa.
Katibu wa Bodi ni Magambo, ambaye ni mkurugenzi mkuu wa mfuko. Kabla ya kuwa mkurugenzi mkuu, Magambo alikuwa mkurugenzi wa mipango, uwekezaji na miradi wa PSSSF.
Mkutano wa bodi uliogoma kuidhinisha fedha hizo ulifanyika tarehe 24 Aprili mwaka huu. Bodi imevunjwa 14 Mei 2026, miezi 14 baada ya kuzinduliwa. Sababu ya kuvunjwa kwa bodi hiyo hazikutajwa.
Hata hivyo, gazeti hili limeelezwa kuwa menejimenti ya PSSSF chini ya Nyansaho na Magambo, imekuwa ikishawishi bodi kuidhinisha mradi huo tokea Novemba mwaka jana.
MwanaHALISI limeshindwa kuwapata Nyansaho na Magambo ili waweze kufafanua sababu za menejimenti kusimamia mradi unaopingwa na bodi kwa maelezo kwamba ni kaburi la mfuko.
Linaendelea kuwatafuta.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya PSSSF, menejimenti imekuwa iking'ang'aniza mradi huo, ambao bodi inashikilia kuwa uwekezaji wake ni sawa na kuzika fedha za umma kutokana na kuwapo uwezekano mdogo wa kuzirejesha, huku wastaafu wakizidi kuongezeka.
"Na sababu hizo, bodi imekuwa ikisisitiza kutokuwa tayari kutoa fedha kwa ajili ya mradi ambao ungeenda kuathiri pia uendeshaji wa viwanja vingine vilivyopo kama Uwanja wa Kimataifa wa Mwanza na Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)," ameeleza mfanyakazi mmoja wa PSSSF.
Anasema, chini ya sheria ya PSSSF ya mwaka 2018, bodi ya wadhamini imepewa mamlaka, chini ya Kifungu cha 9(d) na Kifungu cha 53 kusimamia uwekezaji wa fedha za mfuko.
Anasema, menejimenti inayong'ang'ania uwekezaji huo, imekuwa ikiwahamisha baadhi ya wakurugenzi wanaodaiwa kupinga mradi huo.
Taarifa ya bodi inasema, pendekezo hilo liliwasilishwa kwa mara ya kwanza mbele ya bodi Novemba 2025, lakini lilikataliwa kwa kuwa halikuwa sehemu ya mpango na bajeti ya mwaka 2025/2026 iliyokuwa imeidhinishwa na bodi.
"Bodi haiwezi kukubaliana na pendekezo hili, kwa kuwa hata kiwango cha punguzo cha asilimia 6.5 kwenye uwekezaji kilichowekwa hakikidhi matakwa ya sera ya uwekezaji ya mfuko inayotaka miradi ya aina hiyo kutoa angalau asilimia 16 ya faida," imeeleza sehemu ya taarifa ya bodi.
Hivyo basi, "Bodi imefikia hitimisho kwamba, kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa chini ya Kifungu cha 9(d) na Kifungu cha 53 cha Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma ya mwaka 2018 (Sura ya 371), Bodi haijatoa idhini kwa PSSSF kuwekeza katika mradi huo."