Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Macho yanaongea .. Sura inasema.. The guilty are afraid...! Yaliyomo moyoni mwa mtu akishindwa kuyadhibiti hujitambulisha kwa uwazi kwenye macho na taswira kupitia sura yake!
Furaha
Huzuni
Fadhaa
Sintofahamu
Maumivu
Uoga
Uongo
Ukweli
Bashasha
Kimuhemuhenk
Hali zote hizi huweza kutambuliwa kwa urahisi kupitia utambuzi wa macho na taswira..
Jinsia pinzani ni wepesi sana kuathiriwa na hizi hali za hisia za kiroho.. Katika hali kama hizi si vema kuwapa hadhira aongee lolote ama chochote! Ataharibu! Kwakuwa atataka kujikaza kisabuni na kutaka kuonesha uimara.. Hapo ndio atazidi kutoa boko
Baadhi ya hizo hizo zitakufanya
Ukose nuru usoni
Taswira isawajike
Macho yazamwe ndani
Ngozi ifubae
Ngozi ipate makunyanzi
Macho yakose uimara wa kutazama hadhira
Ana mzigo mzito moyoni
Kachoka
Kazeeka
Hajiamini
Anaugua hata kama haumwi
Amejawa na hamaniko
Ana wasiwasi
Hana amani
Hajioni kama ni yeye yule
Hajisikii wepesi wa ukuu bali uzito na fukuto la kukataliwq😭
Hizi sio hali za kumcheka wala kumdhihaki. Zinatupata sote maishami japo si kwa ukubwq wake
Naamini angetamani arudishe muda nyuma.. Judy Boucher aliimba.. If i can turn back the time..!
Wengi tunakutana na hizi hali kutamani kurudisha wakati nyuma.. Lakini dunia haina kinyume na wakati hauna rivasi
Ulishaharibu kubali kuishi na maumivu ama kubali kutubu na kusimama tena.. Ukijitia kigego na banditu 2026 inakusubiri izidi kukunyoosha na kukutafuna mpaka ikumalize
Kiburi si maungwana.. Happy new year 2026!