Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 3,651
- 11,548
Oct, 11, 2024
"Tunalazimika kupunguza idadi ya wafanyakazi wetu ili kuendana na uhalisi wa hali yetu ya kifedha."
—Kelly Ortberg (Boeing CEO)
—Kelly Ortberg (Boeing CEO)
Wafanyakazi watakaopunguzwa ni 17,000 ambayo ni sawa na 10% ya wafanyakazi wote. Na hii itaathiri wafanyakazi katika ngazi zote kuanzia executives, managers na wafanyakazi wengine.
KUSIMAMISHA UTENGENEZAJI NA UCHELEWASHAJI WA BAADHI YA MATOLEO YA BOEING
Akizungumzia matoleo ambayo wana mpango wa kusimamisha utengenezaji wake, Ortberg alisema Boeing 767 freighter itaachwa kuzalishwa kufikia mwaka 2026 baada ya kumaliza order ya ndege 29 za mteja wa mwisho.
Kumekuwa na kusuasua kwa uzalishaji tangu Sept 13 kufuatia mgomo wa wafanyakazi 33,000 wa kampuni hiyo wakidai ongezeko la mishahara, wakipinga vigezo vipya vya mikataba ya kazi na wengine wakidai retirement benefits. Yote hayo yameifanya Boeing iwe na weak financial position.
Mgomo huo pia umechangia kucheleweshwa uzalishaji wa ndege za 737 Max na 777x iliyopelekea kuchelewesha kufanya delivery kwa wateja wao kwa wakati.

HASARA NA DENI
KITENGO CHA COMMERCIAL JETS
- Kwa sasa Boeing ina deni la $60 billion na kufikia nusu ya mwaka huu imepata hasara ya zaidi ya $7 billion.
KITENGO CHA DEFENSE, SPACE & SECURITY
- Kitengo hiki kimeripoti hasara ya $2 billion. Ikumbukwe hiki ndio kitengo ambacho kilipewa kandarasi na NASA ya kutengeneza Starliner capsule na kuwapeleka wanaanga wawili wa NASA kwenye Kituo cha Anga cha Kimataifa (ISS) na kushindwa kuwarudisha mpaka leo. Boeing inatarajia hasara kubwa zaidi katika kitengo chake cha defense kutokana na mgomo unaoendelea.
UBORA NA USALAMA WA NDEGE ZA BOEING
Bwana Ortbrerg amekiri kuwa kuna shida upande wa ubora na usalama wa ndege zao, na watalifanyia kazi hilo.
"Boeing inaendelea kuzingatia usalama na ubora kwa wateja."
—Kelly Ortberg (Boeing CEO)
—Kelly Ortberg (Boeing CEO)
FIDIA NA FAINI
Wakati hayo yakiendelea mahakama jijini Texas imeitaka Boeing pia kuzilipa fidia familia 346 za wahanga wa ndege zao za 737 MAX zilizopata ajali mwaka 2018 na 2019 kwa sababu ya hitilafu. Boeing wamesema wako tayari kulipa kiasi cha $487 million kwa familia hizo.
Boeing imekubali pia kutumia $455 million kuboresha usalama huku ikisimamiwa na mahakama na waangalizi huru.
MIPANGO YA BOEING YA KUONGEZA MAPATO
Boeing inapaswa kukusanya kitita cha $10 billion kupitia uuzaji wa hisa na dhamana. Je, itawezekana kupata kiasi hicho? Bad news baada ya tangazo la CEO hisa za Boeing zimeshuka katika soko la hisa.
Baada ya U.S automobile industry kupoteza global hegemony kama vile Ford na GM kupoteana kwenye global market,
sasa inaonekana U.S aerospace industry inaenda kuporomoka. Boeing is in turmoil!