Bokoboko la kuku....

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Ngano nzima (shayiri) 3 Vikombe

Kuku ½ (3 LB takriban)

Thomu na tangawizi iliyosagwa 1 kijko cha supu

Pilipili manga ya unga ½ kijiko cha chai

Jiyrah (cumin/bizari ya pilau) ½ kijiko cha chai

Chumvi kiasi

Kidonge cha supu 1

Samli ya moto ½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Roweka ngano (shayiri) tokea usiku au muda wa masaa.

2. Katakata kuku mtie katika sufuria, tia maji kiasi viungo vyote. Mchemeshe awive na ibakie supu yake.

3. Toa kuku, toa mifupa na umchambue chambue vipande vidogo vidogo.

4. Chemisha ngano (shayiri) kwa kufunika sufuria hadi iwive na kukauka maji.

5. Tia supu ya kuku katika ngano (shayiri), na kuku uliyemechambua. Tia kidonge cha supu.

6. Tia samli nusu (bakisha nusu) kisha songa mchanganyiko uchanganye hadi ivurugike kuku na ngano (shayiri) vizuri.
7.weka kwenye sahani na mimina samli imoto ilobakia.
 

Attachments

  • 1384964684312.jpg
    14 KB · Views: 583
We ni mkali ktk sekta hii ya maakuli, Unatisha nakupigia salute.
 
Mie farkhina katika vyakula vilivyonishinda biriyani inachukua namba, nimekula mpaka ya wale wanaosifiwa kwamba ni Wataalam wa kupika biriyani lakini mhhhhh!!! Bokoboko sikujua kama ni mapishi rasmi ya chakula hicho nilidhani mpishi kakosea ndio maana chakula kikaitwa bokoboko, "leo Tamara mkono umeteleza katupikia bokoboko" Nimejifunza kitu leo.
 
Last edited by a moderator:

Hahahahaha sasa biriani imekushindia nini? Labda nkupikie yangu pengine utaipenda lol
Kuna mapishi rasmin yanaitwa bokoboko...very healthy
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK
Hata sijui rafiki na si mimi tu nawafahamu watu wengi tu ukiweka biriyani, pilau na ubwabwa lol!!! basi biriyani ndio itayoguswa na wachache zaidi ukilinganisha na hivyo vingine. Mie nikapata ugali na samaki ya kukaanga na mchicha pembeni na pilipili ya kumwaga basi roho nyeupee lol!!! 🙂🙂

Hahahahaha sasa biriani imekushindia nini? Labda nkupikie yangu pengine utaipenda lol
Kuna mapishi rasmin yanaitwa bokoboko...very healthy
 

Hahahahaha kumbe ujanja wote huo mahanjumati huwezi kula lol....ila kusema ukweli BAK hujala hasa biriani inaitwa biriani....
Cc mimi49....hebu njoo umuambie huyu...
 
Last edited by a moderator:
Asante shostingo. Nna mtihani wa kupika wali wa bokoboko, na haswa kwa sababu wali usipochambuka sili kabisa bora nile ugali.
BAK, inawezekana kuna spices ambazo hupendi kwenye biriani? Mie nna watu wasiopenda spices na biriani yangu inakuwa na spices chache japo vitunguu maji na thomu inakuwa kwa wingi. Try to spare the spices uone.
 
Last edited by a moderator:

Wali bondo? Means wa maji mengi?
Ukiwa hujauzoea mchele au kwa first time kupika kwa vile hujui kiwango cha maji kiasi gani unahitaji...pendelea kuuchemsha kwa maji mengi kidogo ukikaribia kuiva uchuje alafu ukaushe utaendelea kuwiva kwa mvuke...
 
Last edited by a moderator:

Kweli hata mie nimefkiria why hapendi biriani...hapendi spices BAK nadhani...
Hahahaa mie nkipika vyakula vyangu haviwezi kula maana vyengine kama vyanukia kihindi masala yake lol...
Labda chai lol
 
Last edited by a moderator:
Mmmh. Sasa nikishachuja utamu utatoka wapi? Hahaha.
Yaani nasema mie sijui kupika bokoboko. Manake mchele nisioujua naweka maji kidogo tu. Ila kuna mtu ananiambia yeye apenda bokoboko. Na mie huwa sili bokoboko.
Wali bondo? Means wa maji mengi?
Ukiwa hujauzoea mchele au kwa first time kupika kwa vile hujui kiwango cha maji kiasi gani unahitaji...pendelea kuuchemsha kwa maji mengi kidogo ukikaribia kuiva uchuje alafu ukaushe utaendelea kuwiva kwa mvuke...
 
Mmmh. Sasa nikishachuja utamu utatoka wapi? Hahaha.
Yaani nasema mie sijui kupika bokoboko. Manake mchele nisioujua naweka maji kidogo tu. Ila kuna mtu ananiambia yeye apenda bokoboko. Na mie huwa sili bokoboko.

Mie nahisi hautoki utamu ukiuchuja....
Tena hupenda kuuroweka mchele before kuupika kama basmat yazidi kunyooka...
 
Unapoenda kwenye shughuli zile za wenyewe unaambiwa huyu mpishi wa hapa leo ndio bingwa wa kupika biriyani katika jiji la maraha (Dar) unasema haya ngoja leo nijaribu tena kula hiyo biriyani. Si huyo ndiyo bingwa wa kupika biriyani banaaa sasa unategemea hiyo biriyani itakuwa tamu kupita kiasi. Ukija kuitia mdomoni unaishia kusema tu Mhhhh!!!! kama ya bingwa ndiyo hivi basi mie najivua uanachama wa kula biriyani. Sijui banaaaa labda nitakuja kuila mahali siku moja nitaifurahia sana, lakini kuna wapishi wakiamua siku kuingia jikoni wakupikie chochote kile iwe ubwabwa, pilau, mchuzi wa kuku, wa mbuzi, wa kila aina wakupikie mahanjumati ya kila aina, chapati, maandazi, kaimati, na mazagazaga mengine unaweza kujitafuna vidole kuna watu wanapika banaaa!!!! lakini ikija kwenye biriyani Mhhhhh!!! Sasa ukishakula biriyani ya wapishi wawili wazuri sana mmoja unamjua fika na mwingine inadaiwa ni bingwa wa kukaangiza biryani Dar na bado hukufurahia, sijui banaa.

[
QUOTE=King'asti;7871696]Asante shostingo. Nna mtihani wa kupika wali wa bokoboko, na haswa kwa sababu wali usipochambuka sili kabisa bora nile ugali.
BAK, inawezekana kuna spices ambazo hupendi kwenye biriani? Mie nna watu wasiopenda spices na biriani yangu inakuwa na spices chache japo vitunguu maji na thomu inakuwa kwa wingi. Try to spare the spices uone.[/QUOTE]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…