Bokoboko la kuku....

Bokoboko la kuku....

Unapoenda kwenye shughuli zile za wenyewe unaambiwa huyu mpishi wa hapa leo ndio bingwa wa kupika biriyani katika jiji la maraha (Dar) unasema haya ngoja leo nijaribu tena kula hiyo biriyani. Si huyo ndiyo bingwa wa kupika biriyani banaaa sasa unategemea hiyo biriyani itakuwa tamu kupita kiasi. Ukija kuitia mdomoni unaishia kusema tu Mhhhh!!!! kama ya bingwa ndiyo hivi basi mie najivua uanachama wa kula biriyani. Sijui banaaaa labda nitakuja kuila mahali siku moja nitaifurahia sana, lakini kuna wapishi wakiamua siku kuingia jikoni wakupikie chochote kile iwe ubwabwa, pilau, mchuzi wa kuku, wa mbuzi, wa kila aina wakupikie mahanjumati ya kila aina, chapati, maandazi, kaimati, na mazagazaga mengine unaweza kujitafuna vidole kuna watu wanapika banaaa!!!! lakini ikija kwenye biriyani Mhhhhh!!! Sasa ukishakula biriyani ya wapishi wawili wazuri sana mmoja unamjua fika na mwingine inadaiwa ni bingwa wa kukaangiza biryani Dar na bado hukufurahia, sijui banaa.

[
QUOTE=King'asti;7871696]Asante shostingo. Nna mtihani wa kupika wali wa bokoboko, na haswa kwa sababu wali usipochambuka sili kabisa bora nile ugali.
BAK, inawezekana kuna spices ambazo hupendi kwenye biriani? Mie nna watu wasiopenda spices na biriani yangu inakuwa na spices chache japo vitunguu maji na thomu inakuwa kwa wingi. Try to spare the spices uone.
[/QUOTE]

Itakua hujaipenda tu....kila mtu na chakula apendacho usijali kuwa huwezi kula biriani,.....vitamu tele vipo utakula weeee mpaka....
Mwenzenu kwa mara ya kwanza tu nipo age kama 17 nlikula ugali wa muhogo mahali yaani hadi leo chakula kile nakipenda....mkipika mnialike jamani lol
 
  • Thanks
Reactions: BAK
farkhina, mie sikuli basmat kabisaaa labda nikiwa safari na sina ujanja wa kupata mkate na chai. Na mie napenda spices kiasi ila kwenye chai ndo sina huruma nazo. Yaani mie siwezi kunywa chai ya majani na maji pekee. Shurti nichanganye kwanza kila kiungo, mchai chai, tangawizi, iliki na pilipili manga. Sipendi karafuu na mdalasini.
BAK, wewe bana hupendi spices. especially nahisi hupendi mdalasini kama mimi. But unapenda pilau?
 
Last edited by a moderator:

Mie chai hutia mdalasini,zatari,hiliki na majani na mchai chai nkiwa nao...
Karafuu ukiweka kwenye pilau nzuri sana
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Ahsante mamy,napenda shayiri ila nimekula kwa watu tu mie sijawahi kuipika.
Nitaanza na hii W'end.
Utalipwa kheir kwa ilmu.
 
Hahahahaha kumbe ujanja wote huo mahanjumati huwezi kula lol....ila kusema ukweli BAK hujala hasa biriani inaitwa biriani....
Cc mimi49....hebu njoo umuambie huyu...
farkhina huyu ningempa lile biriyani langu lazima lingemlevya kabisa ha ha ha...Angekula mpaka akalala BAK unapitwa jamani.....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ngano nzima (shayiri) 3 Vikombe

Kuku ½ (3 LB takriban)

Thomu na tangawizi iliyosagwa 1 kijko cha supu

Pilipili manga ya unga ½ kijiko cha chai

Jiyrah (cumin/bizari ya pilau) ½ kijiko cha chai

Chumvi kiasi

Kidonge cha supu 1

Samli ya moto ½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Roweka ngano (shayiri) tokea usiku au muda wa masaa.

2. Katakata kuku mtie katika sufuria, tia maji kiasi viungo vyote. Mchemeshe awive na ibakie supu yake.

3. Toa kuku, toa mifupa na umchambue chambue vipande vidogo vidogo.

4. Chemisha ngano (shayiri) kwa kufunika sufuria hadi iwive na kukauka maji.

5. Tia supu ya kuku katika ngano (shayiri), na kuku uliyemechambua. Tia kidonge cha supu.

6. Tia samli nusu (bakisha nusu) kisha songa mchanganyiko uchanganye hadi ivurugike kuku na ngano (shayiri) vizuri.
7.weka kwenye sahani na mimina samli imoto ilobakia.
Mi napenda nile bokoboko na ule mchuzi wa zabibu shost hio samli siwezi!!!!
 
Asante dia

M'badala wa samli ni upi coz hiyo itanishinda
 
Yaa saalaaam bibie farkhina.

Apo kwenye bokoboko umenipatia hswaaa. Thank God najua kulipika, nlijifundisha bcoz my hubby loves it
 
Last edited by a moderator:
farkhina, mie sikuli basmat kabisaaa labda nikiwa safari na sina ujanja wa kupata mkate na chai. Na mie napenda spices kiasi ila kwenye chai ndo sina huruma nazo. Yaani mie siwezi kunywa chai ya majani na maji pekee. Shurti nichanganye kwanza kila kiungo, mchai chai, tangawizi, iliki na pilipili manga. Sipendi karafuu na mdalasini.
BAK, wewe bana hupendi spices. especially nahisi hupendi mdalasini kama mimi. But unapenda pilau?

He he heeeh, Zanzibar yetu inakufaa wewe
 
Last edited by a moderator:
Unapoenda kwenye shughuli zile za wenyewe unaambiwa huyu mpishi wa hapa leo ndio bingwa wa kupika biriyani katika jiji la maraha (Dar) unasema haya ngoja leo nijaribu tena kula hiyo biriyani. Si huyo ndiyo bingwa wa kupika biriyani banaaa sasa unategemea hiyo biriyani itakuwa tamu kupita kiasi. Ukija kuitia mdomoni unaishia kusema tu Mhhhh!!!! kama ya bingwa ndiyo hivi basi mie najivua uanachama wa kula biriyani. Sijui banaaaa labda nitakuja kuila mahali siku moja nitaifurahia sana, lakini kuna wapishi wakiamua siku kuingia jikoni wakupikie chochote kile iwe ubwabwa, pilau, mchuzi wa kuku, wa mbuzi, wa kila aina wakupikie mahanjumati ya kila aina, chapati, maandazi, kaimati, na mazagazaga mengine unaweza kujitafuna vidole kuna watu wanapika banaaa!!!! lakini ikija kwenye biriyani Mhhhhh!!! Sasa ukishakula biriyani ya wapishi wawili wazuri sana mmoja unamjua fika na mwingine inadaiwa ni bingwa wa kukaangiza biryani Dar na bado hukufurahia, sijui banaa.

[
QUOTE=King'asti;7871696]Asante shostingo. Nna mtihani wa kupika wali wa bokoboko, na haswa kwa sababu wali usipochambuka sili kabisa bora nile ugali.
BAK, inawezekana kuna spices ambazo hupendi kwenye biriani? Mie nna watu wasiopenda spices na biriani yangu inakuwa na spices chache japo vitunguu maji na thomu inakuwa kwa wingi. Try to spare the spices uone.
[/QUOTE]

Umenikumbusha dada zangu wa hapo Dar walikua hawapendi mseto wa choroko.

Siku mama yangu aloenda kule akawaambia hamjala mseto nyie subiri niwapikie leo.

Weeee, ama tokea siku hio ilikua kero, wakikaa siku kdg, wanamkera bibi wa Unguja awapikie mseto.

Mapishi yataka tungo.
 
Mapishi yataka tungo.[/QUOTE]

Kabisaaa shosti...
 
Back
Top Bottom