- Thread starter
- #21
Sasa huo mtihani. Afu hembu weka recipe ya kaimati my dear. Wknd nigezee.
Heeee bi shosti mbona ipo hapa tayari...tena nimetaja uje uangalie...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa huo mtihani. Afu hembu weka recipe ya kaimati my dear. Wknd nigezee.
[/QUOTE]Unapoenda kwenye shughuli zile za wenyewe unaambiwa huyu mpishi wa hapa leo ndio bingwa wa kupika biriyani katika jiji la maraha (Dar) unasema haya ngoja leo nijaribu tena kula hiyo biriyani. Si huyo ndiyo bingwa wa kupika biriyani banaaa sasa unategemea hiyo biriyani itakuwa tamu kupita kiasi. Ukija kuitia mdomoni unaishia kusema tu Mhhhh!!!! kama ya bingwa ndiyo hivi basi mie najivua uanachama wa kula biriyani. Sijui banaaaa labda nitakuja kuila mahali siku moja nitaifurahia sana, lakini kuna wapishi wakiamua siku kuingia jikoni wakupikie chochote kile iwe ubwabwa, pilau, mchuzi wa kuku, wa mbuzi, wa kila aina wakupikie mahanjumati ya kila aina, chapati, maandazi, kaimati, na mazagazaga mengine unaweza kujitafuna vidole kuna watu wanapika banaaa!!!! lakini ikija kwenye biriyani Mhhhhh!!! Sasa ukishakula biriyani ya wapishi wawili wazuri sana mmoja unamjua fika na mwingine inadaiwa ni bingwa wa kukaangiza biryani Dar na bado hukufurahia, sijui banaa.
[QUOTE=King'asti;7871696]Asante shostingo. Nna mtihani wa kupika wali wa bokoboko, na haswa kwa sababu wali usipochambuka sili kabisa bora nile ugali.
BAK, inawezekana kuna spices ambazo hupendi kwenye biriani? Mie nna watu wasiopenda spices na biriani yangu inakuwa na spices chache japo vitunguu maji na thomu inakuwa kwa wingi. Try to spare the spices uone.
farkhina, mie sikuli basmat kabisaaa labda nikiwa safari na sina ujanja wa kupata mkate na chai. Na mie napenda spices kiasi ila kwenye chai ndo sina huruma nazo. Yaani mie siwezi kunywa chai ya majani na maji pekee. Shurti nichanganye kwanza kila kiungo, mchai chai, tangawizi, iliki na pilipili manga. Sipendi karafuu na mdalasini.
BAK, wewe bana hupendi spices. especially nahisi hupendi mdalasini kama mimi. But unapenda pilau?
Mi napenda nile bokoboko na ule mchuzi wa zabibu shost hio samli siwezi!!!!Ngano nzima (shayiri) 3 Vikombe
Kuku ½ (3 LB takriban)
Thomu na tangawizi iliyosagwa 1 kijko cha supu
Pilipili manga ya unga ½ kijiko cha chai
Jiyrah (cumin/bizari ya pilau) ½ kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Kidonge cha supu 1
Samli ya moto ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Roweka ngano (shayiri) tokea usiku au muda wa masaa.
2. Katakata kuku mtie katika sufuria, tia maji kiasi viungo vyote. Mchemeshe awive na ibakie supu yake.
3. Toa kuku, toa mifupa na umchambue chambue vipande vidogo vidogo.
4. Chemisha ngano (shayiri) kwa kufunika sufuria hadi iwive na kukauka maji.
5. Tia supu ya kuku katika ngano (shayiri), na kuku uliyemechambua. Tia kidonge cha supu.
6. Tia samli nusu (bakisha nusu) kisha songa mchanganyiko uchanganye hadi ivurugike kuku na ngano (shayiri) vizuri.
7.weka kwenye sahani na mimina samli imoto ilobakia.
Ahsante mamy,napenda shayiri ila nimekula kwa watu tu mie sijawahi kuipika.
Nitaanza na hii W'end.
Utalipwa kheir kwa ilmu.
Ooooooh Habibit Qalbii umekusudia niniiii!!.... Mwenyeezi Mungu Asalimishe mikono yako dadngu na Akukirimu al-Jannat. Bokoboko la century!!

Asante dia
M'badala wa samli ni upi coz hiyo itanishinda