Bokoboko la kuku....

Bokoboko la kuku....

Ngano nzima (shayiri) 3 Vikombe

Kuku ½ (3 LB takriban)

Thomu na tangawizi iliyosagwa 1 kijko cha supu

Pilipili manga ya unga ½ kijiko cha chai

Jiyrah (cumin/bizari ya pilau) ½ kijiko cha chai

Chumvi kiasi

Kidonge cha supu 1

Samli ya moto ½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Roweka ngano (shayiri) tokea usiku au muda wa masaa.

2. Katakata kuku mtie katika sufuria, tia maji kiasi viungo vyote. Mchemeshe awive na ibakie supu yake.

3. Toa kuku, toa mifupa na umchambue chambue vipande vidogo vidogo.

4. Chemisha ngano (shayiri) kwa kufunika sufuria hadi iwive na kukauka maji.

5. Tia supu ya kuku katika ngano (shayiri), na kuku uliyemechambua. Tia kidonge cha supu.

6. Tia samli nusu (bakisha nusu) kisha songa mchanganyiko uchanganye hadi ivurugike kuku na ngano (shayiri) vizuri.
7.weka kwenye sahani na mimina samli imoto ilobakia.

Nimekufuatilia sana katika mapishi yako. Asante sana. Mimi jirani yako kusini tu mwa Toronto. Ombi: Rudisha AVATAR yako ya zamani. Samahani kama nimekuudhi.
 
Hahaaahaaa usijali..bila ya samahani
 
Mie farkhina katika vyakula vilivyonishinda biriyani inachukua namba, nimekula mpaka ya wale wanaosifiwa kwamba ni Wataalam wa kupika biriyani lakini mhhhhh!!! Bokoboko sikujua kama ni mapishi rasmi ya chakula hicho nilidhani mpishi kakosea ndio maana chakula kikaitwa bokoboko, "leo Tamara mkono umeteleza katupikia bokoboko" Nimejifunza kitu leo.
ha haa, karibu pilau la temeke......
leo halijatokea la bbm, lol!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Chezeya pilau la Temeke na pembeni kuna mlenda weye!!!!! unaweza kujitafuna vidole 🙂🙂
ha haaa, ngoja waje wala pilau hapa wakusikie unailia na mlenda....... utajuuutaaaaa.....
mi simo kabisa huko...
ngoja nikajisongee ugali wangu na dagaa wa mawese....... leo nina rahaje! karibu uni-join rafiki yangu, teja mwenzangu.....
wapi Arushaone....... nawe unakaribishwa teja mwenzetu, mpitie na mlongo wangu snowhite kukamilisha team
 
Last edited by a moderator:
Hata mie naona leo una furaha ya ajabu, hongera zako. Furaha huongeza maisha ya binadamu na kuonekana bado ni mdogo wa kustahili kuhudhuria shule ya msingi lol!!!!! hahahaha Ngoja niwapitie hao.

ha haaaa, :tape:
 
Chezeya pilau la Temeke na pembeni kuna mlenda weye!!!!! unaweza kujitafuna vidole 🙂🙂

Pilau la temeke ndio pilau gani BAK?
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Pilau hili ni pilau tamu sana. Walaji walilipenda mno basi mlaji mmoja akadai aliwahi kula pilau tamu kama hilo maeneo ya Temeke, basi tangu siku hiyo pilau linalopikwa na Fixed Point likapewa jina rasmi la pilau la Temeke.

Pilau la temeke ndio pilau gani
BAK
?
 
Last edited by a moderator:
Pilau hili ni pilau tamu sana. Walaji walilipenda mno basi mlaji mmoja akadai aliwahi kula pilau tamu kama hilo maeneo ya Temeke, basi tangu siku hiyo pilau linalopikwa na Fixed Point likapewa jina rasmi la pilau la Temeke.

Hhahahaahahahaha Fixed Point nialike nije kula hilo pilau ya temeke...
 
Last edited by a moderator:
Pilau hili ni pilau tamu sana. Walaji walilipenda mno basi mlaji mmoja akadai aliwahi kula pilau tamu kama hilo maeneo ya Temeke, basi tangu siku hiyo pilau linalopikwa na Fixed Point likapewa jina rasmi la pilau la Temeke.
ha haaa, ntakuwa sikualiki tena kama unanitangazia kwa watu......
xmas inakaribia, unataka nipikie kwenye pipa?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mhhhhhh!!!!! Haya banaaaa basi turudi kwenye ugali na dagaa za mawese, unajua utamu wa hii kitu. Unaweza kula kipindi kirefu tu na bado ukaendelea kutamani tu. Haihusu kitu kupika kwenye pipa maana shughuli yake huwa inakuwa si ya kawaida ukimaliza uko hoi bin taabani.

ha haaa, ntakuwa sikualiki tena kama unanitangazia kwa watu......
xmas inakaribia, unataka nipikie kwenye pipa?
 
farkhina inabidi tu unialike.....diet nitaacha kwanza. Lakini nyinyi waznz mnatuaharibia kiswahili sana, hili sio BOKOBOKO...hili ni HARIS nijuavyo mimi.

Bokoboko ni lile la mchele linaloliwa na mchzi wa zabibu.....nalo tamujeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
 
Sisi hili ndio tunaita Bokoboko...
 
Back
Top Bottom