Bolt kusitisha huduma ya magari kwa wateja binafsi

Bolt kusitisha huduma ya magari kwa wateja binafsi

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Kama wengi wenu mnavyojua, LATRA ilitoa maagizo ya namba LATRA/01/2022 yaliyotolewa tarehe 14 Machi 2022. Licha ya athari za agizo la bei na kamisheni kwa biashara, Bolt imeendelea kutoa huduma za usafiri ili kuonyesha nia njema na kuunda fursa ya azimio la amani.

Hivyo basi, Bolt na LATRA wamekuwa na mawasiliano na majadiliano mengi kutatua suala hilo. Kwa bahati mbaya, majadiliano yamechukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa na hivyo kutoa shinikizo lisilostahili katika uendelevu wa biashara ya Bolt Tanzania.

Madhumuni ya notisi hii ni kuwafahamisha, kama wadau wetu wakuu, kwamba Bolt itakuwa ikifanya mabadiliko ya kiutendaji kuanzia tarehe 17 Agosti 2022. Madadiliko haya yatahusisha kuzuia magari yasitumike kwa abiria wa kawaida bali yatumike tu kwa abiria wa makampuni, yaani wateja wa kadi. Inasikitisha kwamba mabadiliko haya yanaweza kuathiri biashara zako vibaya.

Hata hivyo, Bolt haina chaguo lingine ila kukabiliana na hasara katika soko hadi tuone uboreshaji mkubwa katika mfumo wa biashara kuelekea sekta ya usafirishaji ili kuunda hali ya ushindi pande zote miongoni mwa madereva, wasimamizi wa sekta ya usafiri na abiria.

Tunatumai kuwa changamoto hizi zitatatuliwa ili uendelee kujitafutia riziki.

Bolt Tanzania

PIA SOMA: Meneja Afrika Mashariki: Bolt inaweza kusitisha huduma Tanzania
 
Kama wengi wenu mnavyojua, LATRA ilitoa maagizo ya namba LATRA/01/2022 yaliyotolewa tarehe 14 Machi 2022..
Wengine hata hatuijui bolt ni nini na inafanyeje kazi!Ufafanuzi tafadhali kwa faida ya wengi wasio ijua kama mimi.
 
Kama wengi wenu mnavyojua, LATRA ilitoa maagizo ya namba LATRA/01/2022 yaliyotolewa tarehe 14 Machi 2022. Licha ya athari za agizo la bei na kamisheni kwa biashara, Bolt imeendelea kutoa huduma za usafiri ili kuonyesha nia njema na kuunda fursa ya azimio la amani.
Ruto oyeee
 
shida iko wapi kwani mkuu

mbona kama unatishia nyau

yaani unaongea as if watu wanasafiri bure
 
Bolt kwa madereva inawaumiza sana, makato yao ni makubwa kupita kiasi, inafikia hatua ambayo dereva ukimuita anamaliza trip kabla ya safar alaf bei mnamalizana kwa mazungumzo.
 
Back
Top Bottom