Bomba la mafuta kati ya Tanzania na Uganda lakabiliwa na changamoto za kisheria

Bomba la mafuta kati ya Tanzania na Uganda lakabiliwa na changamoto za kisheria

Shing Yui

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
15,168
Reaction score
38,049
Wataalamu wa sheria hebu tasaidieni

=====

Bomba la mafuta kati ya Uganda na Tanzania lakabiliwa na changamoto ya kisheria.

Mashirika manne yasiyo ya kiserikali yamekwenda kwenye mahakama ya Afrika Mashariki ili kuzuia ujenzi wa bomba la mafuta la Afrika Mashariki EACOP uliofanywa na Uganda na Tanzania.

Katika kesi iliyowasilishwa Novemba 6, mashirika hayo manne yanakosa amri ya Uganda na Tanzania, ili kuhakikisha mambo yanayofuata yafanywe kabla ya ujenzi wa mirai yoyote yanayofanana: tathmini ya athari zitakazoletwa kwa mabadiliko ya hali ya hewa, tathmini ya athari zitakazoletwa kwa haki za binadamu, ushauri wa hadhara wenye ufanisi na uwazi ambao unaweza kushirikishwa na jamii na umma.

Mashirika hayo yasiyo ya kiserikali sasa yanatafuta marufuku dhidi ya Uganda, Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki kujenga bomba la mafuta linalopita hifadhi za wanyamapori.

Imefahamika kwamba bomba litasafirisha mafuta ya asili kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, Tanzania.

FB_IMG_16064795474021597.jpg
 
Mabeberu wameanza tena baada ya kuona mbinu imefeli kwa Lisu. Wamwajiri Lisu awe wakili kwenye hiyo kesi.
Sisi tupo na Mungu, mbinu zao chafu za kishetani zitafeli tu!
 
Hayo mashirika yaliyoenda mahakamani lazima yatakuwa kutoka hapo jirani kwa nya. Ng'au!

Bila kupinga mtazamo wako, huo mradi upo kweli au ni ngonjera kama zile za sarafu ya pamoja ya East Afrika? Maana mwanzo huo mradi ulizinduliwa kwa Mikogo huko Chongoleani Tanga 2017, na ikasemekana kufikia 2020 utaanza kazi rasmi. Lakini mpaka leo ni porojo, mpaka juzi alivyokuja Museveni kwenye kampeni, ndio wakawa wanahadaa umma kama kuna huo mradi.

Huyo Museveni ni tapeli kama tapeli mwingine, nakumbuka aliwahi kuomba apewe sehemu katika bandari ya Tanga na Mkapa ili awe anasafirishia mizigo ya Uganda, na kweli akapewa, mpaka leo hajawahi kupeleka hata matofali mabovu. Kwangu nahisi ni mradi wenye utata zaidi, maana hilo bomba walishakubaliana na Kenya lipitie huko, mara likahanishiwa Tanzania. Wakati ule wa uzinduzi niliwahi kusema Nina mashaka na huo mradi, maana museveni ni mtapeli, na kweli hayo yako wazi.
 
Hili nalo litapita Kama mradi wa umeme wa bwawa la mwl nyerere
 
Mpo na Mungu wapi? Acheni kuhusisha Mungu kwenye mambo ya kipumbavu
Usijitoe ufahamu, kumbuka kipindi cha COVID 19, tulishinda kwa Maombi. Chadema waliungana na mabeberu wao kwa hila za kishetani. Tukashinda
 
Back
Top Bottom