Watanzania Awamu hii imetufanya wote kuwa wajinga ili kutafuta teuzi kwa sababu mamlaka ya kuteua inatumia mbinu ya kuangalia usoni wa kuteua au kuwasikia sanasana kusaidia hata ujinga. Bomba linalosemwa litaleta maendeleo ni la Waganda, mafuta yatakayopita humo ni ya Waganda na mafuta hayatakuja Tanga bali yatapita hapo kwenda kwa wateja wa Waganda kokote duniani yatakakonunuliwa. Bomba litaacha wananchi wanalia kote litakakopita maana mashamba yao yatachukuliwa na nyumba kubomolewa kwa maendeleo ya Waganda. Mafuta yenyewe yatakuwa ghafi hata wezi (Watanzania wote siku hizi tunasifika kwa utaalamu huo) hawatanufaika maana yatakuwa hayajasafishwa na nchi yetu haina kiwanda baada ya TIPER cha Dar es Salaam kufa. Bomba la Mafuta la TAZAMA la Zambia liko nchini sasa karibu miaka 50 labda wenzetu wa Chato watatwambia mchango wa Bomba hilo kwenye maendeleo ya Wilaya, Mkoa, Kanda hata maendeleo ya wakulima waliopitiwa na Bomba hilo.