Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 130
- 368
katika kikao hicho kitaongozwa na Wawaziri January Makamba na kuhudhuriwa na Innocent Bashungwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mhandisi Hamad Y. Masauni ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani. Kwa upande wa serikali ya Zambia, kikao kitahudhuriwa na Ambrose L. Lufuma Waziri wa Ulinzi, Jacob J. Mwiimbu- Waziri Mambo ya Ndani na Peter C. Kapala Waziri wa Nishati.
Kikao kazi kinalenga kutatathmini utekelezaji wa masuala ya ulinzi na usalama wa bomba la mafuta la TAZAMA kama ilivyokubalika katika kikao cha kwanza cha Wizara hizi tatu kilichofanyika mwezi Desemba, 2022 hapa Dar es Salaam baada ya Serikali ya Zambia kuamua kutumia bomba hili kusafirisha mafuta safi badala ya mafuta ghafi (crude oil). Bomba la TAZAMA lina urefu wa KM 1,710 kutoka Kigamboni – Dar es salaam hadi Indeni - Ndola Zambia. Changamoto kubwa ni ulinzi na usalama wa bomba hilo baada ya kuanza kusafirisha mafuta yaliyosafishwa badala ya mafuta ghafi.
Katika kikao cha kwanza, kulikuwa na makubaliano ya mikakati mbalimbali itekelezwe ikiwemo ushirikishwaji wa wanavijiji katika sehemu ambapo bomba linapita.
Aidha, katika kikao kazi hiki kutajadiliwa pia namna ya upanuzi wa bomba hili kwa ajili ya kupitisha aina zote za mafuta safi na jinsi ambavyo mikoa ya kusini mwa nchi yetu inaweza kupata mafuta kupitia bomba hili na pia bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Tanzania kwenda Zambia. Tathmini ya upanuzi wa bomba ili kuwezesha kupitisha aina zote za mafuta ikiwemo tathmini ya bomba la gesi asilia inaendelea. Ujenzi utaanza mara baada ya tathmini hii kukamilika.