Wakumpongeza hapa ni Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli aliyenunua madege ya Magufuli, akaanzisha ATCL badala ya ATC, akateua CEO na watendaji Wakuu na akateua Bodi ya Wakurugenzi, kwa kutotoa agizo toka juu, huwa ni Sheria, dege moja liwapeleke Simba. Pia pongezi zimwendee CEO ambaye hakujipendekeza kwa aliyemteua kuruhusu Simba wapelekwe Nigeria kwenda kufungwa na kurudi wakilalamika Uwanja haukuwa mzuri. ATCL ina madege aina tatu, ya kwanza Bombardier inachukua abiria 75, ya pili Airbus inachukua 130 na ya tatu Dreamliner inachukua 262, aina zote tatu zinauwezo wa kufika Abuja na kurudi. Simba inakwenda Abuja, Nigeria na wachezaji 11 watakaocheza na kufungwa kwa dakaki 90 tu na kugeuza kurudi wakiimba kujisifu walivyocheza vizuri ingawa wamefungwa kwa sababu ya Uwanja. Kenya Airways na Ethiopian moja kwa moja au kwa kuunganisha zina safari za kawaida kwenye ruti hiyo na nauli kwa kila abiria hata ATCL wanaijua kwa sababu ni ya IATA. ATCL ni Shirika la Safari za Anga na madege yake ni ya abiria lakini halitoi huduma kwenye ruti hiyo ingawa madege yapo yamepark yakingoja safari lakini yanaweza kukodishwa. Simba wanatakiwa kwenda Mwanza na wachezaji 11 basi lao limeharibika wanakodi basi la Musukuma Bus Service la abiria 65 lakini Simba wanakwenda na wachezaji 11 tu washangiliaji wanachama wao watawakuta huko. Musukuma nauli yake ni sh. 30,000 kwa kiti anadai sh. 1,950,000 kwa viti 65 na kwa kuwa Simba wamekodi basi lote wanakubali kulipa na kwenda kufungwa wakilalamika Uwanja wa Kirumba siyo mzuri. Yanga wanapeleka timu ya wachezaji 11 Mwanza kwa mchezo wa Jumamosi kwa basi la Musukuma walikopata nafasi maana madege yamepark mpaka wiki ijayo maana yanaenda mara moja tu kwa wiki yakingoja kwenda London na China. Vichwa vya wanaCCM visivyo na akili kabisa vinataka Serikali yao ingeruhusu madege matupu yatumike kupeleka wawakilishi wao kwa gharama zozote ingawa ndege mbadala zipo. Yanga wanalipa nauli sh. 330,000 na kucheza kama Pele!