As long as tumebinafsisha viwanda vyetu na kutochukua hatua za kuhakikisha kuwa wale waliokabidhiwa viwanda hivyo wanaendeleza shughuli za viwanda badala ya kuvibadilisha kuwa go-down tutaendelea kuwa na tatizo la ajira. Hebu niulize hivi serikali ina sera gani kuhusu viwanda na inachukua hatua gani kuhakikisha viwanda vilivyobinafsishwa vinafufuliwa? Kwa nini mpaka leo hatujajiuliza ilikuwaje Mwalimu Nyerere aanzishe viwanda karibu katika mikoa yote ya Tanzania, na licha ya kwamba vilikufa kutokana na uzembe wetu, sijamsikia mwanasiasa yeyote anayezungumzia sababu zilizopelekea kufa kwa viwanda hivyo na tunachopaswa kufanya. Hatuwezi kutegemea wawekezaji ndio wawe vyanzo vya ajira kwa vijana wetu. Serikali lazima iweke mkakati na msisitizo katika ufufuaji wa viwanda ama sivyo tutaendelea kulitizama hili bomu la ajira kwa vijana likituripukia.
Mkuu Jasusi, point muhimu sana hizi. Niongezee senti thumuni.
Tatizo la ajira tunaliona sasa na tunasahau kuwa huko nyuma lilikuwa kubwa pia.
Hatua za kutawanya viwanda(kwa maana ya viwanda vya nchi zetu) ilifanyika makusudi kabisa, kwanza kuzuia massive urbanization na pili kutoa opportunity kwa watu na wazalishaji wa sehemu husika, na mwisho kuinua maisha ya watu wa eneo husika
Karibia kila kanda ilikuwa na kitu cha kusaidia. Ninakumbuka chuma, mbolea, sabuni kule nyumbani Tanga, Mwanza na viwanda vya nguo na uchambuaji wa pamba ikiwa ni pamoja na mafuta, Morogoro, Arusha, Korosho Mtwara n.k.
Viwanda hivi vilitoa ajira kwa wananchi wote bila kuchagua mfanyakazi au mkulima kwasababu yote yanategemeana.
Soko la ndani lilikuwepo na bado lipo. Tanganyika packers walitumia Ng'ombe wa Shinyanga n.k. Je, ng'ombe hakuna kiasi cha kusema kiwanda kimekosa malighafi. Je, walaji hakuna kiasi cha sisi kuagiza nyama kutoka Brazili.
Kwanini basi Tanganyika packers ilikufa, au kiwanda cha maturubai n.k.
Endapo soko hakuna kwanini leo tuuziwe betri feki za kutumia siku moja, kwanini leo tuagize mitumba, kwanini leo tuagize vineriti kutoka Afganistan na Pakistani. Kwanini mafuta ya kulia yatoke Malaysia na kwanini sisi ni soko kubwa la EAC.
Tulikuwa na soko zuri la nje, tatizo letu tunadhani soko ni lazima liwe la Ulaya. Tuli export nguo kwa majirani zetu, General tyre ilikuwa ni kipusa, betri za Matsushita zilikuwa hot cake Kenya kwa uchache sana wa kutaja mifano.
Tulipoua viwanda tukamwathiri mkulima moja kwa moja. Pamba sasa inauzwa ''raw' kwa thamani ndogo, viwanda vya uchambuzi vimekufa, mazao yatokanayo kama mafuta ya pamba hakuna tena.
Matokeo ya yote hayo ni sub standard zilizojaa kutoka China tena zikitengenezewa uani.
Nadiriki kusema tulifika mahali ambapo tulitakiwa tuwekeze katika technology ili tuwe competetive katika world stage hata kama ni third world.
Privitization haikuweza kuepeukika kwasababu ilikuwa ni new world order chini ya IMF, WTO, WB n.k
Wala sioni tatizo na privitization. Tatizo ninaloliona ni kukosekana kwa leadership na political will.
Hili ndilo lilitengeneza loophole ya greedy and covetous leaders kugeuza mali za taifa kuwa maghala kama kule Mang'ula.
Sasa Wapogoro wa Zignal na Kidodi wanahamia mijini kutafuta mkate.
Kibaya zaidi haya yakitendeka hao wanaotabiri ukubwa wa bomu in order to score political point walikuwa ndio waandaji wa sera za kugeuza mali zetu kuwa maghala!
Elimu, hili nalo tutalijadili.