Bomu la Nyuklia: Jielimishe hapa

Bomu la Nyuklia: Jielimishe hapa

formula ya kutengezea nyuklia

formula E = mc*2
 
Mk_6_nuclear_bomb.jpg

Kitu cha mrusi hicho, kinaitwa Tsar Bomb. Ni bomu lenye nguvu zaidi
 
Nasikia Bomu la Hydrogen lina nguvu kubwa zaidi kuliko hata hilo la nyuklia wanaloliogopa? wenye kufaham watujuze?
 
Ninaanzisha thread hii ili kuwakaribisha wataalamu wa Nuclear phyiscis watupe elimu kuhusu Nuclear energy.

Bomu la nyuklia hutengenezwa kutokana na madini yenye asili ya Radioactive kama vile Uraninum au Plutonium. Madini haya yana tabia kuwa yakistuliwa kidogo tu basi yanaanza process inayoitwa nuclear fission ambapo hupasuka vipande vidogo vidogo huku yakiwa yaanaachia joto jingi sana.

Madini ya uranium yana mifumo (isotopes) mbili, Uranium U-235 na Uranium U-238. Mfumo wenye nguvu za nuklia nie ule wa U-235, hata hivyo madini ya uranium ya asili kama yanayochimbwa hapa kwetu yana kama nusu asilimia tu ya U235, wakati asilimia karibu 99.5 ni U-238.

Bomu moja la Nyukilia huhitaji U-235 kama kilo hamsini hivi hivi, kwa hiyo ili kuzipata hizo kilo hamsini inabidi uwe na uranium asili zaidi ya tani mia moja halafu uichuje kwa kutumia chekecheo ziitwazo centrifuge ili kuondoa U-238 ambayo ni nzito kidogo na kuacha U235 ambayo ni nyepesi. Kuchuja tani moja ya Uraniuma inaweza kuchukua miaka miwili au hata mitano kutegemea na ubora wa centrifuge ulizo nazo.

Ukishaweka U235 iliyochujwa mahali palipotulia, unachohitaji ni kuidisurtb kidogo tu hata kwa kuiangushia mchanga, halafu yenyewe inaaza nuclear fission inayosababisha kitu kinaitwa chain reaction ambayo hutoa joto kali sana na kuunguza kila kiliocho hapo katika maeneo yake. Nguvu za nuklia hutumia joto hilo badala ya makaa ya mawe kuchemsha maji kutoa mvuke wa kuendesha mashine za kufua umeme.

Yale mabomu ya atomiki yalioangusha Nagasaki na Hiroshima yaliuwa watu kwa sababu ya joto ikafikia hata mifupa ya watu ikiwa inayeyuka kwa sababu ya joto. Mabomu conventional yanayotumia baruti huua watu na kubomoa majengo kwa ajili ye pressure lakini Nyuklia huwasha moto tu.

Wana fizikia wa nuklear physiscs ingieni hapa mtupe elimu kuhus nishati hii inayoogopwa duniani kote.

Naomba kuongezea kidogo. Kutokana na ukuaji wa mbinu, uelewa na teknolojia katika Nuclear weapons, specifications hizo (katika highlighetd blue) ni basics na zinaweza zikawa si standard tena au kuna modification nyingi zaidi kwa sasa.

Aina ya nuclear bombs haiko moja bali kadhaa kutokana na jinsi yanavyokuwa designed na mchanganyiko wa elements ili kuleta ile chemical reaction. Zaidi umegusia fission weapons lakini pia kuna fusion weapons na zote hizi ni nuclear bombs. Wakati fission (atomic bomb) inahusisha zaidi splitting au kugawanyika kwa atom ya Uranium au Plutonium, meanwhile fusion weapon (hydrogen bomb) inajumuisha process mbili fission na fusion, process ya kwanza inatumika "kulipua" ya pili na hii ya pili (fusion) ni pale atom zinapoungana kuunda moja kubwa. Kwa maana rahisi ni kwamba bomu la atomic linakuwa detonated na linalipuka (nuclear fission) ndani kwa ndani katika shell yake na kusababisha (compressing, heating) bomu jingine la hydrogen lililomo ndani yake kuanza nuclear fusing na kulipukia nje. Katika aina ya pili ya nuclear bomb elements nyingine nyingi ukiacha Uranium isotopes zote U-238 na U-235 pamoja na Plutonium zinatumika zikiwemo isotopes tofauti za hydrogen na kwa mpangilio maalum unaounda chain reaction.

Umesema U-238 haina umuhimu katika uundaji wa bomu lakini katika fusion weapon U-238 inatumika vizuri kama kiungo kinachozidisha nuclear fission reaction ikianza. Kwa hiyo katika aina ya pili ya nuclear bomb (yenye fission + fusion) elements ambazo ziko stable zinaweza kuwa destabilized (mfano hydrogen) na mwisho nuclear reaction ikazaa nishati kubwa na kuwa hatari sana na kiasi tu cha unstable elements kama U-235 kinatumika kama sehemu ya bomu hilo.
 
Nasikia Bomu la Hydrogen lina nguvu kubwa zaidi kuliko hata hilo la nyuklia wanaloliogopa? wenye kufaham watujuze?

Mkuu bomu la nuclear lina aina tofauti kutokana na muundo, hivyo hydrogen bomb bado pia ni bomu la nuclear. Aina kuu mbili za bomu la nuclear ni ile ya atomic bomb au fission weapons na ile ya thermonuclear bomb au hydrogen bomb au fusion weapon. Nimeelezea kidogo tofauti hapo post ya juu.
 
fo[SUP][/SUP]rmula ya nyuklia E=mc[SUP]2[SUP] [/SUP][/SUP]
 
Hivi ni nchi gani inayoongoza kwa utengenezaji wa mabomu ya nyuklia duniani???

Countries with the biggest nuclear weapon stockpiles:
1. Russian federation 2. Usa 3. France 4. China 5. Uk 6. Pakistan 7. India 8. Israel 9. South Korea
 
Hana lolote huyo VIP Bilal kitabu gani kaandika
Tujifunze kuheshimu Elimu ya wenzako hata kama mnatofautiana kisiasa

Kuandika kitabu hakukufanyi wewe kuwa ni mzuri

Watanzania tunapenda kujifanya kila kitu tunajua ndio yale yale wa Tundu Lissu anayemsema chenge hajui sheria wakati Chenge mwenzake ni Kichwa cha Havard

wapo watakaokurupuka na kuhoji na kusema Chenge Hamna kitu
 
Mmmh! umenikumbusha mbali sana "terminologies" hizo. Mara nuclear fusion, isotopes e.t.c. Mimi hapa cna msaada kwakweli (zaid ya "likes" na kuwafagilia kina Gay-Lussac!, bhaaas!).

Natamani Dr.Ghalib Bilal (V.President) angekuwa humu ndani. Ni moja ya watanzania nadra sana wenye Elimu & Kisomo cha mambo haya.

Respect!


Naskia huyu mzee skinhead the nouma sana..
 
Countries with the biggest nuclear weapon stockpiles:
1. Russian federation 2. Usa 3. France 4. China 5. Uk 6. Pakistan 7. India 8. Israel 9. South Korea

Vp Iran, maana naona UNSC wanamuandama sana juu ya nuclear.
 
Interesting topic indeed.... Mi mjinga mkubwa kwenye haya madude
 
Vp Iran, maana naona UNSC wanamuandama sana juu ya nuclear.

Kama umemuelewa vizuri mtoa mada ni kwamba nuclear energy ina matumizi mengi ikiwamo kuzalisha umeme, kuendesha mitambo mikubwa nk. Case ya Iran ni kwamba kwa sasa wao wanarutubisha tu uranium hawajaanza matumizi yake, hofu inakuja kwa UNSC kwamba watakapomaliza au watakaporutubisha kiasi cha kutosha itatatumika ktk matumizi sahihi kwa maana ya kufua umeme au kuendesha mitambo na si nuclear weapons.
 
Kama umemuelewa vizuri mtoa mada ni kwamba nuclear energy ina matumizi mengi ikiwamo kuzalisha umeme, kuendesha mitambo mikubwa nk. Case ya Iran ni kwamba kwa sasa wao wanarutubisha tu uranium hawajaanza matumizi yake, hofu inakuja kwa UNSC kwamba watakapomaliza au watakaporutubisha kiasi cha kutosha itatatumika ktk matumizi sahihi kwa maana ya kufua umeme au kuendesha mitambo na si nuclear weapons.

mkuu Mvella jr. kama unachoongea ni kuwa hao ndugu (IRAN) ishu yao kubwa si nuclear weapons bali ni mahitaji ya kufua umeme, kwanini hao UNSC wawe na hofu tena ?
hofu imatoka wapi akati mtu anamipango mizuri na nchi yake ?
au mimi ndiyo cjakuelewa ?

.made in mby city.
 
Last edited by a moderator:
Tujifunze kuheshimu Elimu ya wenzako hata kama mnatofautiana kisiasa

Kuandika kitabu hakukufanyi wewe kuwa ni mzuri

Watanzania tunapenda kujifanya kila kitu tunajua ndio yale yale wa Tundu Lissu anayemsema chenge hajui sheria wakati Chenge mwenzake ni Kichwa cha Havard

wapo watakaokurupuka na kuhoji na kusema Chenge Hamna kitu

Kwanza hii topic haihusiani na mtu au elimu yake, topic ni NUCLEAR BOMB, haya ya kuwataja watu au mtu na elimu yake sidhani kama hapa ni mahala pake! Kama hujui chochote kuhusu topic bora kukaa kimya, hayo ni mawazo yangu.
 
Countries with the biggest nuclear weapon stockpiles:
1. Russian federation 2. Usa 3. France 4. China 5. Uk 6. Pakistan 7. India 8. Israel 9. South Korea
Not south,it is north korea.
na si big stockpile.
 
  • Nuclear power plants use "nuclear fission" (the process of splitting an atom in two). "Nuclear fusion" (the process of combining atoms into one) has the potential to be safer but has not yet been developed to operate within a large power plant.
  • Nuclear energy comes from uranium, a nonrenewable resource that must be mined.
  • Every 18 to 24 months, a power plant must shut down to remove its spent uranium fuel, which becomes radioactive waste.
  • 13% of the world's electricity comes from nuclear power plants that emit little to no greenhouse gases.
  • Nuclear energy is being used in more than 30 countries around the world and even powers Mars rovers.
 
Back
Top Bottom