Paulsylvester
JF-Expert Member
- Oct 15, 2021
- 1,464
- 3,379
Tangu kuondokewa kwa aliyekuwa Amiri Jeshi na Rais wa Tanzania wa awamu ya Tano Mh JPM
Mitandaoni kote hakujawahi kutulia, nilidhani labda kwa kuwa nchi yetu haijawahi kukumbwa na kadhia hiyo ya Rais kufa akiwa madarakani, ndiyo maana kila mtu anajaribu kuongea lakwake, na kifo chake, wengi hawakuamini, kwa sababu ilikuwa ni ghafla mno
Lakini kwa kuwa mwenye kuamua mtu awe hai au hapana ni Mungu na Siri hizo anazo yeye peke yake, Watanzania tulilipokea, ingawa kwa huzuni na majonzi makubwa, na kifo chake na kuagwa kwake, kulionyesha kuwa ni mtu aliyekuwa ameshiba mioyoni mwa watu!
Nilijipa matazamio kwamba, kwa muda angalau wa nusu Mwaka, tungeliweza kusahau na maisha yakaendelea, lakini ninachokiona kuwa itatuchukua muda mrefu mno na hata kutufikisha sehemu si salama ni hii mijadara inayoendelea kila uchwao mitandaoni
Mijadala hii ina pande mbili, kuna wale wanaompondea kwa sana na kumsema kwa ubaya na dhihaka kubwa licha ya kwamba nao pia ni binadamu wale wale waliokwenye mawindo ya aliyewaumba na kwa muda wowote aweza kuwachukua, lakini madai yao ni kwamba waliumizwa mno na utawala wake kiasi kwamba hawataki wanyamaze, hili najiuliza, Je, ipo faida wanapata wakimsema?
Lakini kundi la pili ambalo haliamini hivyo kama wale wa kundi la mashambulizi kudai kwamba waliumizwa, wao wanaona aliyekuwa kipenzi chao kwa nini anasemwa vibaya licha ya kwamba hayuko ktk dunia hii na wanataka wasahau angalau kuangalia maisha mengine, ila kunapotokea mmoja akimsema vibaya JPM, mioyo yao inaumia, na wanaamini kiongozi wao alifanya mengi mno mazuri na aliwagusa maisha yao
Na ukifuatilia mjadara unaoendelea sasa, utagumdua kuwa, kuna waka moto ktk mioyo ya makundi haya!!
Ni ombi langu kwa Serikali, mjadara kumhusu JPM ufungwe rasimi, utazaa mengine mabaya zaidi na nchi yetu itaingia kwenye historia mbaya zaidi,
Mbaya zaidi ni kuwepo watu wanaodai kifo cha JPM ni cha utata, haya mambo yakilelewa lelewa ni hatari,
Tumefika mbali sasa kwa dalili hizi, kwamba mtu Fulani asionekane kanda Fulani??
Chonde chonde, Serikali inaouwezo wa kuzuia Bomu hili lisilipuke
Kwa nini tunagawanyika kwa sababu tuu ya kilichoamliwa na mmiliki wa watu wote..?