Bondia afariki baada ya kupigwa KO katika shindano la ndondi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Maswali yanaulizwa kuhusu taratibu za usalama katika ndondi ya Zimbabwe kufuatia kifo cha Taurai Zimunya baada ya kupigwa katika pambano mjini Harare.

Zimunya, 24, wa uzito wa Super bantam, alifariki siku ya Jumatatu, baada ya kuzimia wakati wa pambano lisilo la ubingwa siku ya Jumamosi.

Ni mara ya kwanza kwa bondia kufariki nchini Zimbabwe kutokana na majeraha aliyoyapata ulingoni.

Lawrence Zimbudzana, katibu mkuu wa Bodi ya Kitaifa ya Kudhibiti Ndondi na Mieleka ya Zimbabwe (ZNBWCB), anasema kuwa mipango ya uchunguzi bado haijashughulikiwa.

"Kwa sasa tutaangazia mazishi, na kisha tuketi na kuangalia masuala," Zimbudzana aliambia BBC Sport Africa katika mazishi ya Zimunya Jumatano.

Taarifa iliyotolewa na ZNBWCB ilisema kuwa "taratibu zote muhimu za matibabu zilifuatwa na msaada wa dharura wa matibabu ulitolewa mahali hapo kabla ya kupelekwa hospitali".

Zimunya alipigwa makonde kadhaa kichwani kabla ya kubanduliwa nje katika raundi ya tatu ya pambano la raundi sita.

Aliyekuwa mkufunzi wake Tatenda Gada alihuzunika, akihisi nyota huyo alikuwa na uwezo mkubwa.

"Tumeopokonywa mojawapo ya matarajio yetu mazuri," Gada alisema. "Nilifanya kazi na Taurai kwa zaidi ya miaka minne - nilimtazama akistawi na alikuwa mmoja wa nyota wajao katika fani hii."

Babake Zimunya, Samson, alikuwa bondia mahiri asiye wa kulipwa na alitarajia mwanawe angebeba jina la ukoo na kuwa bingwa.

Ndondi ilikuwa imerejea tu Zimbabwe baada ya vizuizi vya kupambana na janga la corona kulegezwa.
1.jpg
 
View attachment 1998019View attachment 1998019View attachment 1998019
Kuna makonde yamebeba kifo ndani yake.. Ndondi ni mojawapo ya michezo hatari ya kishetani.. Imagine watu wanachonganishwa wapigane
 
Zanzibar hakuna huo ujinga. Mzee Karume alipiga marufuku kabisa. Haiwezekani mchezo uwe wa chuki, mnapigana bila kugombana.
 
Yani unamuumua mwenzio uso, unamvimbisha mwenzio macho, unamng'oa mwenzio meno bila ganzi, unampelekea mwenzio kichapo mpaka anakata network, halafu unasema ni mchezo? Bora huku Zanzibar tumeupiga marufuku.
 
Jamaa alikuwa anarusha ngumi kama mawe mwenzake anaonekana amekata network ila bado anamkandamiza za kutosha 🐒
 
Hao jamaa hugeuka wanyama kwa muda wanapokuwa ulingoni
Nilishawahi kupitia kidogo mafunzo ya boxing na kucheza tu boxing wakati wa mazoezi aisee ukimpata wa kumuonea ukianza kumtupia makonde kuna raha fulani unaipata bila muamuzi makini ni rahisi sana kuua au kumletea mwenzako madhara makubwa
 
Back
Top Bottom