Bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo(23) amchakaza mzungu

Safi sana, bondia Hassan Mwakinyo,jamaaa yuko vizuri kwenye combination Taifa limsapoti kaleta heshima kubwa Sana.
 
Aisee huyu ni namba nyingine. Hata pigano analopigana siyo la uchochoni. Main event ni kati ya Amir Khan vs Samuel Vargas. Na ana miaka 23 tu. Watangazaji nguli wa Sky wamemsifu sana.
Anatakiwa aungwe mkono kafanya vizuri, hapo wanahitajika waziri wa habari na waziri wa utalii kumpa sapoti ya kifedha na kumtangaza na kuitangaza nchi kwa mali na vitendea kazi.
 
Kapigana na mtu mwenyewe amekondeana hivyo, ndiyo kujisifu!!...akutane na jitu kama Amir khan uone 😀😀😀
Bora unyamaze Kama hujui mambo ya ngumi, si kila unachoona useme bwana,!we unafikiri wanapigana bila kujua uzito gani? Wabongo ndo maana wengi hamuendelei.
 

Hii habari yako ungetoa neno Niko hapa London , maana unatifanya sisi wa huku Ushirombo tukuonee wivu...[emoji276] [emoji276]
 
Mtanzania mwenye umri wa miaka 23 hassan mwikinyo amshushia kipigo kikali mzungu huko uingereza.

Sina maneno mengi nyie angalieni vidio tu.

=====

BONDIA Hassan Mwakinyo wa Tanzania jana amefanikiwa kushinda kwa Technical Knockout (TKO) sekunde ya 45 raundi ya pili dhidi ya Muingereza, Sam Eggington Uwanja wa Arena Birmingham, zamani Barclaycard Arena mjini Birmingham, England.

Katika pambano hilo lisilo la ubingwa uzito wa Light Middle, Mwakinyo alimzidi kabisa mpinzani wake tangu mwanzo kabla ya kummaliza katika raundi ya pili kuelekea pambano kuu jana kati ya Muingereza, Amir Khan na Samuel Vargas Colombia anayeishi Canada.

Khan aliyeshinda kwa pointi za majaji wote, alimuangusha Vargas mwanzoni mwa raundi ya pili, naye akaangushwa mwishoni mwa raundi hiyo wote waliinuka haraka kuendelea hadi kumaliza raundi.

Khan aliyemuangusha Vargas na raundi ya tatu pia pamoja na kumjeruhi pua, kwa ushindi huo anaweza kupigana na Manny Pacquiao au Kell Brook.
Na Mwakinyo baaada ya ushindi huo wa jana atapanda tena ulingoni Oktoba 20, kuzipiga na mwenyeji Wanik Awdijan ukumbi wa Alex Sportcentrum mjini Nuremberg, Ujerumani katika pambano la kuwania taji la vijana la IBF uzito wa Middle.

Pambano la jana lilikuwa la tatu Mwakinyo anapoigana nje ya Tanzania akiwashinda kwa mara ya pili baada ya kumshinda pia kwa TKO Anthony Jarmann wa Namibia Agosti 8, mwaka jana ukumbi wa Grand Palm Hotel mjini Gaborone nchini Botswana.
Desemba 2, mwaka jana Mwakinyo alipoteza kwa pointi mbele ya mwenyeji, Lendrush Akopian ukumbi wa Krylia Sovetov mjini Moscow, Urusi.
 

Attachments

hahahaaa. nimeiona jana aisee hatari sio kwa kupigwa vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…