Bongo movie hazifundishi ujasiri bali msisitizo upo kwenye mahusiano

Artifact Collector

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
6,617
Reaction score
10,205
Kama ulishawah angalia bongo movie hata kwa uchache wake utagundua bongo movie hazifundishi ujasiri kabisa visa vyao karibia vyote ni vya mapenzi hii imepelekea kuwa na kizazi ambacho sio majasiri

Tanzania hatuna majasiri kabisa hii ni kwa sababu mtoto anakua katika mazingira ambayo hayamfundishi ujasiri mojawapo ni hii bongo movie ambapo ukienda kuanzia azam, dstv mpaka startimes familia ziko bize kuziangalia kila siku

Ukiangalia movie za hollywood mfano prison break na hobbit zile movie zinafundisha ujasiri kwa kiasi kikubwa sana movie zetu wajifunze kutengeneza movie zinazofundisha ujasiri na sio kujikita kwenye mahusiano tu
 
Akili zenyewe wanazo za mapenzi mapenzi tu, akili za kufundisha ujasiri wazitoe wapi? Ndio maana muvi zao zinawadodea hakuna wa kuzihitaji. Kwani nani hajui mapenzi tangu azaliwe?
 
Kama ulishawah angalia bongo movie hata kwa uchache wake utagundua bongo movie hazifundishi ujasiri kabisa visa vyao karibia vyote ni vya mapenzi hii imepelekea kuwa na kizazi ambacho sio majasiri

Tanzania hatuna majasiri kabisa hii ni kwa sababu mtoto anakua katika mazingira ambayo hayamfundishi ujasiri mojawapo ni hii bongo movie ambapo ukienda kuanzia azam, dstv mpaka startimes familia ziko bize kuziangalia kila siku

Ukiangalia movie za hollywood mfano prison break na hobbit zile movie zinafundisha ujasiri kwa kiasi kikubwa sana movie zetu wajifunze kutengeneza movie zinazofundisha ujasiri na sio kujikita kwenye mahusiano tu
Watanzania si majasiri Kwa asili
 
Ukitaka kuangalia Bongo Movies angalia Bongohoodz
 
Kama ulishawah angalia bongo movie hata kwa uchache wake utagundua bongo movie hazifundishi ujasiri kabisa visa vyao karibia vyote ni vya mapenzi hii imepelekea kuwa na kizazi ambacho sio majasiri

Tanzania hatuna majasiri kabisa hii ni kwa sababu mtoto anakua katika mazingira ambayo hayamfundishi ujasiri mojawapo ni hii bongo movie ambapo ukienda kuanzia azam, dstv mpaka startimes familia ziko bize kuziangalia kila siku

Ukiangalia movie za hollywood mfano prison break na hobbit zile movie zinafundisha ujasiri kwa kiasi kikubwa sana movie zetu wajifunze kutengeneza movie zinazofundisha ujasiri na sio kujikita kwenye mahusiano tu
Kuliko niangalie huba au jua kali ni bora niangalie our story au unfaithful

Wabongo mapenzi hawayawezi na kila siku wapo bize na movie za mahaba
 
Bongo muvi karibia zote maudhui yao yanafanana! Kila star lazima aigize kumiliki kampuni, nyumba kali, gari kali, mlinzi wa getini lazima aigize kuwa fyatu kichwani!

Tofauti na hapo, basi ni zile za kutumia mazingiria ya maeneo ya pembezoni mwa mji, kuigilizia!

Mtu anajifanya anaishi kijijini, halafu mwili mzima umejaa tattoo! Nywele zimepakwa rangi!! Mwanaume unakuta masikioni ana hereni!!

Kiukweli Bongo muvi wanachoweza ni kudinyana tu wenyewe kwa wenyewe wakati wa kufanya shooting. Ila ukija kwenye ubunifu, ni 0.
 
Hivi kuna Watu bado wanakaza mafuvu yao kuangalia Bongo movies?

Marehemu Kanumba pekee ndiye aliyeshawishi kuangalia muvi za kibongo sababu ya ubunifu?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Kwa sasa wanajitahidi mnyonge mnyongeni haki yake mpeni,kuna waandaaji wapya kweny game wanafanya vizuri,kuna watu wako vizuri kucritisaizi bongo movie na si wafuatiliaji wa tamthilia wala movie wamekariri bongo movie ni kanumba pekee,binafsi skuwa napenda kuangalia bongo movie kabisa ila kwa ss mm ni shabiki mkubwa wa tamthilia ya ZAHANATI YA KIJIJI naipenda sana wanaigiza uhalisia Na ndio tamthilia pekee ninayofatilia ,kila mmoja kafit kwa nafasi yake ,ILA ILE TAMTHILIA ya JERAHA Spendi RAY anavoigiza kizamani
 
Back
Top Bottom