Juzi waziri wa elimu nchini Kenya Profesa Magoha aliponea chupuchupu kupigwa kalamu kwasababu ya kumdhalisha mdogo wake(Director wa Elimu Gatuzi la Uasin Gishu) kwa matusi tu na maneno makali. Najaribu kuwaza ingekuwaje kama angedhubutu kutumia kiboko au fujo kama huyo waziri nchini Tz. Hawa majirani zetu hawajielewi kabisa. Wataishia tu kwenye domo domo za uoga uoga mitandaoni ila hawawezi kuonesha hamaki zao wazi wazi kwa vitendo .
SERIKALI imewatimua nchini raia wawili wa China kwa kosa la kuwatwanga makonde na kuwanyanyasa Watanzania walioajiriwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Chunya Makongorosi mkoani Mbeya, inayojengwa kwa kiwango cha lami.