Bongo Star Search Waache Human Abuse, BASATA na TRCA wawaangalie !

Bongo Star Search Waache Human Abuse, BASATA na TRCA wawaangalie !

NguoYaSikuKuu

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
681
Reaction score
1,020
Nimekuwa naangalia hiki kipindi cha Bongo Star Search karibuni ila Kauli chafu na maneno wanayowapa hawa vijana sio sawa kabisa.
Sijajua kama hizi lugha zingeeleweka huko mbele kwa nchi za wenzetu katika ulimwengu uliostarabika.

Nimeangalia vipindi vingi sana kama hivi mfano American Idol , The Voice na America's Got Talent ila sijawahi kuona kauli chafu za majaji.

Mfano Judge Salama ni jaji anayeongoza kwa kauli chafu na zinazowanyima kujiamini hawa vijana. Master Jay naye ni kinara wa lugha chafu zisizo na staha.

Sijui kama TCRA na BASATA wanafuatilia hiki kipindi vizuri au ndo yale yale ya bora liende.

Nawasihi BASATA an TCRA wawaambie hawa watu wenye hii program wasiwafanye hawa vijana kama vile ni watumwa katika nchi yao. Wanafanywa kama vikatuni .
 
Hapa bongo watu wengi sana wana stress za maisha. Sasa kila mtu hua anatumia ajira yake kama sehemu ya kutolea stress na kumalizia hasira na machungu aliyo nayo, hasa pale ambapo kapewa "rungu". Mfano mwalimu atataka amalizie stress zake kwa wanafunzi, nesi atataka amalizie stress kwa mgonjwa, trafiki atamalizia stress kwa dereva, Salama atatolea stress kwa washiriki wa BSS nk.
 
Ukweli ni kwamba huwa ni kuwapotezea vijana wetu muda tu na sema ni vile pia hakuna ajira kwa sasa ila kuna kauli chafu sana na za kukatisha tamaa kutoka kwa hawa majaji uchwara kisa tu wao wana majina na nafasi, nilitegemea baada ya harmonize kuwachana kweny ile nyimbo yake wangebadirika ila bado wako vilele
 
Huyo Salama anatumia lugha mbaya na maneno ya ovyo mno! Ni kama hajakua, ni sawa na mtu ambaye hana exposure, anaropoka, anapanic halafu ana kaubabe flani ka kishambaaaaaa
Nimeshangaa sana ni kama vile anaona akiwa humble atapoteza brand yake. Anaropokea vijana vibaya sana.
 
Hapa bongo watu wengi sana wana stress za maisha. Sasa kila mtu hua anatumia ajira yake kama sehemu ya kutolea stress na kumalizia hasira na machungu aliyo nayo, hasa pale ambapo kapewa "rungu". Mfano mwalimu atataka amalizie stress zake kwa wanafunzi, nesi atataka amalizie stress kwa mgonjwa, trafiki atamalizia stress kwa dereva, Salama atatolea stress kwa washiriki wa BSS nk.
yaaani , Too much mkuu inabidi wadhibitiwe au kama vp waache hii program.
 
Ukweli ni kwamba huwa ni kuwapotezea vijana wetu muda tu na sema ni vile pia hakuna ajira kwa sasa ila kuna kauli chafu sana na za kukatisha tamaa kutoka kwa hawa majaji uchwara kisa tu wao wana majina na nafasi, nilitegemea baada ya harmonize kuwachana kweny ile nyimbo yake wangebadirika ila bado wako vilele
BASATA wanawachekea ila ni udhalilishaji wa kiasi kikubwa. Naona wanahisi wasipotmia kauli kali kipidi chao kitapungua mileage ila ni ujinga sana.
 
Sasa unategemea nini kutoka kwa mtu kama Salama? Hajulikani ni wa kike au wa kiume, mzee au kijana. Yani kapo kapo tu.
Tatizo la Bongo ni kukosa weledi wa mambo. Unamchukua mtangazaji ambae sifa pekee iliyomtambulisha ni kuwa na chuki kwa kudhihaki kazi za watu (rejea kipindi cha Salama miaka ya 2000) ndio awe judge sasa unatarajia nini toka kwake zaidi ya chuki. Anaona sifa kudhalilisha watu.

Ni vile tu hii ni Bongo na kila kitu kinaenda tu ila ingekuwa nchi za mbele wangepigwa na lawsuits mpaka wasijue pa kupumulia.
 
Back
Top Bottom